Azam FC kuwafuta machozi Watanzania
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Klabu bingwa Afrika mashariki na kati Azam FC usiku wa saa 1:15 wanatelemka uwanjani kuwavaa Mbabane Swallors ya Swaziland mchezo wa raundi ya kwanza kombe la Shirikisho barani Afrika.
Mechi itapigwa katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi na vijana wa Azam wanataka kuwafuta machozi Watanzania hasa baada ya wawakilishi wengine wa Tanzania Dar Young Africans jana kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Azam FC, Jaffari Iddi Maganga amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mtanange wa leo na wamepanga kushinda ili kuwafuta machozi Watanzania, "Tunataka kushinda ili tukae katika mazingira mazuri ya kutinga hatua ya makundi", alisema Iddi ambaye alikuwa mtangazaji wa Radio One