HABARI NJEMA KWA MASHABIKI WA YANGA, KUREJEA KWA MASTAA WAO
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Hizi ni habari njema hasa kwa mashabiki wa Yanga hasa baada ya daktari wa kikosi hicho Edward Bavu kuanika taarifa njema kwa afya za wachezaji muhimu wa kikosi cha kwanza ambao walikosekana kwenye kikosi cha kwanza baada ya majeraha ya muda mrefu na mfupi.
Bavu ameanika afya ya mshambulizi raia wa Zimbabwe Donald Dombo Ngoma kuwa sasa anaweza kurejea uwanjani kwenye michezo ijayo ukiwemo wa marudiano dhidi ya Zanaco ya Zambia.
Mbali na Ngoma, Amissi Tambwe na Thabani Kamusoko nao wako fiti kabisa na huenda katika mchezo wao dhidi ya Zanaco utakaochezwa Jumamosi ijayo kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam nyota hao watacheza kama kocha George Lwandamina ataamua kuwapanga katika kikosi chake.
Hizo ni taarifa njema kabisa kwa mashabiki wa Yanga kwani kikosi hicho kilionekana kupungua makali hasa baada ya kushindwa kuwatumia nyota hao, Lakini hata hivyo Yanga haikuteteleka kwani iliweza kuifunga Kiluvya United mabao 6-1 na kuingia robo fainali ya kombe la Tff