Mdaula United wasaka timu ya kucheza nayo Dar
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Timu ya Mdaula United ya Mdaula wilayani Chalinze mkoani Pwani iko katika mchakato wa kusaka timu ya kucheza nayo mechi ya kirafiki itakapoanza ziara yake ya kimichezo jijini Dar es Salaam.
Kocha na mhamasishaji wa Mdaula United, Shaaban Kipresha ameiambia Mambo Uwanjani kwa simu kuwa vijana wake ambao wanashiriki Ligi Daraja la tatu mkoani Pwani wanataka kuwasili Dar es Salaam ambapo wanahitaji angalau mechi moja kabambe ya kujipima nguvu.
"Ni kweli tunakuja Dar es Salaam hasa baada ya kumaliza ziara yetu hapa Mlandizi, tumecheza na Mlandizi Worriors na kushinda _4-3 mchezo wa kirafiki, lengo letu tuje Dar na tucheze mechi moja ya kirafiki na timu yenye ushindani", alisema Kipresha mchezaji wa zamani wa Baghdad na Big Bonn zote za Magomeni Mikumi jijini Dar es Salaam