Taifa Stars mpya yatangazwa, Kessy ndani
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza kikosi chake kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki.
Stars inaweza kucheza na kati ya Zambia au Rwanda ama timu nyingine yoyote kwakuwa kumekuwa na taarifa tofauti.
Lakini kikosi cha Mayanga kitaongozwa na nahodha wake Mbwana Ally Samatta anayekipiga nchini Ubelgiji katika klabu ya KRC Genk na pia kina vijana wengi zaidi.
Kikosi hicho ni kama ifuatavyo:
Makipa
Aishi Manula (Azam FC), Deogratus Munishi "Dida" (Yanga SC), na Said Mohamed (Mtibwa Sugar).
Mabeki
Shomary Kapombe (Azam FC), Hassan Kessy (Yanga SC), Mohamed Hussein "Tshabalala" (Simba SC), Gardiel Michael (Azam FC), Andrew Vincent (Yanga SC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Erasto Nyoni (Azam FC).
Viungo
Ni Himid Mao (Azam FC), Jonas Mkude (Simba SC), Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC), Frank Domayo "Chumvi" (Azam FC), Muzamiru Yassin (Simba SC), Simon Msuva (Yanga SC), Shiza Kichuya (Simba SC), Farid Mussa (DC Tenerife ya Hispania) na Hassan Kabunda (Mwadui FC).
Washambuliaji
Mbwana Samatta (KRC Genk ya Ubelgiji), Thomas Ulimwengu (AFC Eskillstuna ya Sweden), Ibrahim Ajibu (Simba SC), Mbaraka Yusuph (Kagera Sugar) na Abdulrahaman Mussa (Ruvu Shooting)