Yanga yashindwa kuing' oa Simba kileleni
Na Ikram Khamees. Morogoro
Winga Simon Msuva ameshindwa kuiweka kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kukosa penalti Yanga ikishindwa kuondoka na pointi tatu katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Timu hizo zilitoshana nguvu baada ya kutoka sare tasa ya 0-0 na kuofanya Yanga kuambulia pointi moja inayowasogeza kidogo ikifikisha pointi 53 nyuma ya Simba kwa tofauti ya pointi mbili.
Yanga sasa itakuwa na kibarua kingine Jumatano ijayo itakapocheza na Kiluvya United mchezo wa kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup