Jeshi la Azam mguu sawa Swaziland
Na Mrisho Hassan. Mbabane
Kikosi cha Azam FC kesho kinajitupa uwanjani kurudiana na Mbabane Swallors ya Swaziland mchezo wa hatua ya 32 bora ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Azam FC inaingia uwanjani ikiwa na mtaji wa bao moja ililolipata Uwanja wa Azam Complex zilipokutana katika mchezo wa mkondo wa kwanza.
Mchezo wa kesho Azam inahitaji sare ya aina yoyote na ikivuka kigingi hicho itaumana na moja kati ya timu zilizoondolewa kwenye Ligi ya mabingwa Barani Afrika, Azam itamtegwmea zaidi winga Ramadhan Singano ambaye ndiye aliyefunga bao katika mchezo wa kwanza