Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2017

Manara amlilia Kessy Yanga

Picha
Na Shafih Matuwa. Dar es Salaam Afisa Habari wa Klabu ya Simba Haji Sunday Manara amemsikitikia mlinzi wao wa zamani Hassan Ramadhan Kessy kwa kuendelea kusugua benchi kwenye kikosi cha Yanga hivi sasa na kushindwa kumshawishi kocha Mzambia George Lwandamina ili ampange. Manara aliyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo alidai kuwa Kessy aliihama Simba kwa kebehi akilalamika kwamba Simba ilishindwa kumtimizia ahadi yake. Mchezaji huyo alisajiliwa na Yanga kwa utata mkubwa kwani mkataba wake na Simba ulikuwa bado haujakwisha kitendo kilichozua sekeseke lililopelekea Simba kushitaki TFF ambapo Yanga walitakiwa kuilipa Simba shilingi Milioni 50. Lakini maisha ya beki huyo ndani ya Yanga yanaonekana kama magumu kwani amekuwa akisoteshwa benchi kila mara huku Juma Abdul akicheza karibu mechi zote kuanzia kombe la Mapinduzi, Ligi Kuu Bara, kombe la FA na michuano ya kimataifa na Manara anasema Kessy atajuuta

Ally Kiba, Diamond Platinumz waitwa kamati ya Serengeti Boys

Picha
Waziri wa Habari, Michezo, Utamaduni na Wasanii Nape Moses Nnauye ametangaza majina ya watu kumi kuunda kamati ya kuhamasisha ushiriki wa Tanzania katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ambapo Serengeti Boys itashiriki kwenye fainali hizo zitakazofanyika Gabon. Katika uteuzi wake, Mhe Nape mbali ya kumteua Mwesigwa Celestine kuwa katibu wa kamati hiyo aliwateua wasanii wa muziki wa kizazi kipya Ally Kiba na Diamond Platinumz. Wengine walioitwa kwenye kamati hiyo ni Beatrice Singano, Charles Hilaly, Eric Shigongo, Maulid Kitenge na wengineo ambao mbali na kusaidia uhamasishaji kwa timu hiyo ya Serengeti Boys ili iweze kupatiwa misaada mbalimbali ya kifedha ili ishiriki vema pia mjadala wa Tanzania kushiriki Olimpiki nao ulijadiliwa

HUYU HAPA NDIYE ALIYEIKATA UMEME YANGA

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Kama mlidhania Justin Zulu wa Yanga ndiye mkata umeme peke yake basi mnajidanganya, Said Hamisi Ndemla ndiye aliyeikatia umeme Yanga na kupelekea kuchapwa mabao 2-1 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Huo ulikuwa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, katika mchezo huo Yanga ndio walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza lililofungwa na Simon Msuva kwa mkwaju wa penalti baada ya Obrey Chirwa kuangushwa kwenye eneo la hatari, goli hilo lilipatikana dakika ya 6 kipindi cha kwanza. Yanga walitawala dakika 35 za mwanzo kabla ya Thabani Kamusoko hajaumia na kutolewa nje, benchi la ufundi la Simba SC lilimtoa Juma Luizio na kumwingiza Said Ndemla ambaye aliubadili mchezo na Simba kuuwasha moto na kuelekea mapumziko wakiwa na matumaini kibao. Kipindi cha pili Simba waliendeleza moto na kuliandama lango la Yanga kama nyuki, kuingia kwa nahodha wao Jonas Mkude kuliendeleza moto na kufanikiwa kusawazisha bao na kuongeza la ushindi, mabao ya Simba yalifungwa na ...

Bila ya Ranieli, Leicester yaifumua Liverpool 3-1

Picha
Leicester City wamejikokota na kupanda hadi nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya kuizaba Liverpool kwa mabao 3-1. Leicester walionyesha kiwango cha juu na magoli mawili kutoka kwa Jamie Vardy na moja kutoka kwa Danny Drinkwater yaliididimiza Liverpool. Wakicheza chini ya kaimu kocha Craig Shakespeare aliyechukua mikoba ya Claudio Ranieli, mabingwa hao wa England walicheza kama mabingwa watetezi. Goli la kwanza la Jamie Vardy limekumbusha mtindo waliokuwa wakicheza msimu uliopita, baada ya pasi murua kutoka kwa Marc Aibrighton iliyomfikia Vardy. Magoli hayo ya Leicester ndio magoli ya kwanza kwa klabu hiyo kufunga mwaka huu wa 2017. Liverpool ambao wangeweza kupanda hadi nafasi ya tatu iwapo wangepata ushindi, sasa wamepoteza mechi tano kati ya saba walizocheza katika michuano yote

BARA LA AFRIKA KICHEKO KOMBE LA DUNIA 2026

Picha
Rais wa shirikisho la soka duniani (Fifa) Giani Infantino amesema kuwa bara la Afrika litapewa nafasi 7 katika upanuzi wa timu zitakazoshiriki fainali za kombe la dunia mwaka 2016. Infantino amesema kuwa shirikisho hilo limeongeza uwekezaji wake Afrika kutoka dola milioni 27 hadi 94 kwa mwaka ili kusaidia kukuza mchezo huo, Infantino kwa sasa yuko ziarani nchini Ghana kwa siku moja. Amekuwa akikutana na rais Akufor Addo na maafisa wakuu wa shirikisho la soka nchini Ghana kuzungumzia hatua za kukuza soka nchini humo, Ziara yake ni mojawapo ya ziara za mataifa kadhaa wanachama wa Fifa

Yanga waapa kula sahani moja na Simba kileleni, kuvaana na Ruvu, J,tano

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajia kuendelea tena Jumatano ijayo ambapo mabingwa watetezi wa taji hilo, Yanga SC itawaalika Ruvu Shooting kwenye mchezo utakaofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Yanga wameapa kuifukuzia Simba kileleni na wameahidi kushinda mchezo huo ili kuwapoza mashabiki wake baada ya Jumamosi iliyopita kufungwa 2-1 na Simba, mbali na mchezo huo mmoja wa Jumatano, ligi hiyo itaendelea siku ya Jumamosi Machi 4 mwaka huu Simba itacheza na Mbeya City Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Ukiacha mchezo huo, michezo mingine ya Jumamosi Machi 4, mwaka huu itakuwa ni kati ya Toto Africans na Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, huku Kagera Sugar ikiikaribisha Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Azam FC pia itacheza na Stand United ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Chamazi, Mchezo huo utaanza saa 1:00 jioni wakati mechi nyingine zitaanza saa 10:00 jioni. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeire...

Bossou aigomea Yanga, kisa mshahara

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Mlinzi wa kimataifa wa Togo, Vincent Bossou (Pichani) amegoma kukipiga Yanga akidai mshahara wake wa mwezi Januari, mlinzi huyo alimkatalia kocha Mzambia George Lwandamina kucheza dhidi ya Simba Jumamosi iliyopita katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Taarifa ambazo Mambo Uwanjani imezinyaka kuwa Bossou alikataa kucheza mechi hiyo dhidi ya Simba ambapo Yanga iliweza kulala 2-1, ukuta wa Yanga ulisimamiwa na :Mhandisi' Kevin Yondani na Vincent Andrew 'Dante' na ukaruhusu mabao hayo yaliyowekwa kimiani na Mrundi Laudit Mavugo na Shiza Kichuya. Kwa maana hiyo Bossou atakosekana kwenye mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara ambapo Yanga itacheza na Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Bossou anaidai Yanga mshahara wa mwezi Januari na kwa mujibu wa Katibu mkuu wa Yanga Charles Mkwasa kuwa Bossou peke ndiyo hakulipwa Januari kwakuwa alikuwa nje ya nchi. Bossou aliungana na timu ya taifa ya Togo ilikwenda kushiriki fainali za Mataifa ya Af...

Mkwasa asema Yanga haina fedha kwa sasa

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Katibu mkuu wa Yanga SC Charles Boniface Mkwasa amefunguka mazito na kudai sababu ya kuboronga kwa kikosi chake kilipocheza na Simba na kufungwa mabao 2-1 juzi katika Uwanja wa Taifa jijinj Dar es Salaam. Mkwasa ambaye kitaaluma ni kocha, amesema Yanga ina matatizo ya kifedha kwa sasa hasa baada ya mwenyekiti wake Yusuf Manji kuandamwa na misukosuko na serikali na kupelekea kufungwa kwa akaunti zake zote. Licha ya kufungwa kwa akaunti hizo za Manji ambaye pia ni mfadhili wa timu hiyo, Mkwasa amedai Yanga haitashindwa kumudu gharama za kambi na usafiri na wamejidhatiti kutetea ubingwa wao wa Bara. Yanga ilikubali kichapo cha mabao 2-1 toka kwa mahasimu wao Simba Jumamosi iliyopita kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Yanga ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na Simon Msuva kwa penalti dakika ya sita kipindi cha kwanza. Simba walisawazisha kupitia kwa Laudit Mavugo na kuongeza la ushindi kupitia kwa Shiza Kichuya, hata hivyo Simba wali...

Manchester United watwaa EFL

Picha
Mashetani Wekundu Manchester United wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya EFL baada ya kuilaza Southmpton mabao 3-2 katika mchezo wa fainali katika Uwanja wa Wembley, London. Mabao yaliyoipa ushindi Manchester United iliyochini ya mkufunzi Jose Mourinho yaliwekwa kimiani na Zlatan Ibramovic "Cadabla" (Mawili) dakika ya 19 na 87 na lingine lilifungwa na Jesse Lingard dakika ya 38. Wakati ya Southmpton yalifungwa na Manolo Gabbiadini yote mawili katika dakika za 43 na 48 hilo likiwa taji la kwanza la Mourinho tangu ajiunge Man United msimu huu

Pacquiao kuzichapa na Khan Aprili

Picha
Bingwa wa ndondi uzani wa WelterWeight duniani Manny Pacquiao, atapigana na Muingereza Amir Khan tarehe 23 Aprili mwaka huu. Pambano hilo litaandaliwa baada ya mashabiki wa Pacquiao kwenye mtandao wa Twitter kumchagua Khan kama mwanamasumbwi ambaye wangependa apigane na Mfilipino huyo. "Hiki ndicho mashabiki walikuwa wanataka", Pacquiao mwenye umri wa miaka 38 alisema. Khan wa umri wa miaka 30 alithibitisha pigano hilo licha ya Pacauiao kusema kuwa huenda pigano lake likaandaliwa katika miliki ya nchi za Kiarabu, eneo litakaliandaliwa bado halihatangazwa. Akiongea kwa njia ya video Khan anasema Uingereza, Dubai au Marekani ni kati ya sehemu ambapo pambano hilo likafanyika. Pigano la mwisho la Khan lilifanyika mwezi Mei mwaka 2016, wakati alimsginda kwa Knock out raia wa Mexico Saul "Canelo" Alvarez

Kamusoko atajwa kipigo cha Yanga jana

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Baada ya Yanga SC kuchapwa mabao 2-1 na hasimu wake mkuu Simba SC jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara takwimu mbalimbali zimetolewa na wataalamu wa mambo ya soka. Juma Mwambusi ambaye ni kocha msaidizi wa Yanga ametoboa kilichoiua Yanga jana kuwa ni kuumia kwa kiungo wake Mzimbabwe Thabani Kamusoko, Kocha huyo wa zamani wa Tanzania Prisons na Mbeya City zote za mkoani Mbeya amedai Kamusoko ndiye aliyewadhibiti mno viungo wa Simba. "Kwakweli jana tumepotea pale alipotoka Kamusoko baada ya kuumia, nina hakika kama asingetoka kwa kuumia basi kipindi cha pili tungeendelea kuutawala mchezo na tungeshinda", anasema Mwambusi alipohojiwa na Mambo Uwanjani leo kuelezea mchezo wa jana. Yanga wanajipanga kwa mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa Jumatano ijayo kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam ukiwa ni mchezo wake uliosalia mkononi ili kutimiza mechi 23 sawa na vinara wa ...

Simba yapeleka maafa Jangwani

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Simba SC jioni ya leo imefanikiwa kuilaza Yanga SC mabao 2-1 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu Bara. Yanga walionekana kuutawala mchezo katika dakika 20 za mwanzo kipindi cha kwanza na waliandika bao la kuongoza lililofungwa na Simon Msuva kwa mkwaju wa penalti kufuatia Obrey Chirwa kukwatuliwa kwenye eneo la hatari. Yanga waliendelea kuliandama lango la Simba lakini kocha wa Simba alifanya mabadiliko ya kumtoa Juma Luizio na kumwingiza Said Ndemla ambaye aliweza kuubadili mchezo na Simba kutakata, hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele. Kipindi cha pili Simba walianza kwa spidi na kulitia msukomsuko lango la Yanga na kufanikiwa kusawazisha kupitia Mrundi Laudit Mavugo "King Loud" na kuongeza la pili lililofungwa na Shiza Kichuya. Simba sasa wamefikisha pointi 54 wakiwa mbele kwa tofauti ya pointi tano na wapinzani wao Yanga ambao wana pointi 49 wakicheza mechi 22 wakati...

Asiye na mwana abebe jiwe, Simba vs Yanga

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Wafalme wa soka nchini Simba na Yanga wanakutana jioni ya leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Maneno mengi yamesemwa hasa kutoka kwenye vijiwe mbalimbali lakini mwisho wa siku imetimia ile tarehe iliyopangwa kukutana miamba hiyo, mechi ya leo ni ya marudiano baada ya Oktoba 1 mwaka jana kuumana katika uwanja huo huo wa Taifa na kutoka sare ya kufungana 1-1. Amissi Tambwe alitangulia kuipatia Yanga bao la kuongoza dakika ya 26 kipindi cha kwanza na Simba wakasawazisha dakika ya 87 kipindi cha pili likifungwa na kiungo Shiza Kichuya kwa kutumbukiza kona iliyokwenda moja kwa moja wavuni. Kwa maana pambano la leo linatafuta mbabe wa msimu huu, iwe Yanga au Simba mmoja anaweza kuchomoza na ushindi, Lakini Simba wana kumbukumbu nzuri ya kuchomoza na ushindi wa mikwaju ya penalti kule Zanzibar. Simba iliifunga Yanga kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya kumaliza dakika 90 0-0 mchezo wa nusu fainali kombe la ...

Messi aipeleka Azam robo fainali FA Cup

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Goli pekee lililofungwa na kiungo mshambuliaji Ramadhan Singano "Messi" lilitosha kabisa kuwaua Mtibwa Sugar na kuipeleka robo fainali Azam FC katika mchezo wa kombe la Azam Sports Federation Cup au maarufu FA Cup kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi. Mchezo ulikuwa mkali na wa aina yake kwa timu zote kuonyeshana upinzani ambapo Azam FC ilionekana kucheza vema kwa kipinsi kirefu kabla ya Mtibwa Sugar inayonolewa na mchezaji wake wa zamani Zuberi Katwila haijatawala dakika 20 za mwisho. Azam ilianza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la mapema dakika ya 6 likifungwa na Messi ambaye aliwahi kuichezea Simba misimu miwili iliyopita, Messi aligongeana vema na Salum Abubakar "Sure Boy" ambaye aliendeleza kiwango kizuri katika mtanange huo. Mabingwa hao wa Ngao ya Jamii na Kombe la Mapinduzi waliendeleza kasi yao ili kusaka mabao zaidi lakini safu ya ulinzi ya Mtibwa Sugar ilikuwa makini kumdhibiti mshambuliaji pekee aliyekuwa...

Nitabakia Manchester United- Rooney

Picha
Nahodha wa Uingereza Wayne Rooney amesema kuwa atasalia katika Klabu ya Manchester United baada ya kuhusishwa na uhamisho wa kwenda China. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 amesema kuwa anatumai kwamba atashirikishwa kikamilifu katika mechi zilizosalia za klabu hiyo msimu huu. Mkufunzi wa United Jose Mourinho amekataa kukana kwamba Rooney huenda akaondoka klabu hiyo mwezi huu, japokuwa uhamisho huo huenda usikamilike kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho nchini China mnamo tarehe 28 Februali. "Ni wakati wa furaha kubwa katika klabu hii na ningependa kusalia", alisema Rooney. Wakala wake Paul Stretford alisafiri kuelekea China kuona iwapo atafanikiwa kupata makubaliano japokuwa haijulikani alizungumza na klabu gani. Mbili kati ya klabu tatu zilizoonekana kuwa klabu mbadala ni Beijing Guoan na Jiangsu Suning zikifutilia mbali uvumi kuhusu uhamisho huo wa Rooney

WEMA SEPETU AJIUNGA CHADEMA

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Kada na mwanachama wa Chama Cha Mapjnduzi (CCM) Wema Isaack Abraham Sepetu sambamba na mama yake mzazi kwa pamoja wamejiunga rasmi na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA. leo. Wema ameamua kukihama CCM chama ambacho alikipigania katika uchaguzi mkuu uluofanyika mwaka 2015, Wema ambaye ni msanii wa filamu na Miss Tanzania wa zamani, ameamua kuachana na CCM kutokana na kukandamizwa kwa demokrasia na uhuru wa kuongea. Hivi karibuni msanii huyo maarufu alifikishwa mahakamani akituhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya, Wema alitajwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Poul C Makonda, kwa kitendo hicho ambacho kilimfanya mlimbwende huyo kulala mahabusu Central kwa siku nne kumelekea kuachana na CCM ingawa yeye mwenyewe amesema ameamua kukihama kutokana na kukandamizwa kwa demokrasia. Nao Chadema wamesema wamempokea Wema kwa mikono miwili na wamewataka na watu wengine walioko CCM kumuiga Wema kwani wakati muafaka ni huu, Tayari wasanii kama Joseph M...

Mwamuzi wa Simba na Yanga huyu hapa

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Hatimaye mwamuzi atakayezihukumu Simba na Yanga kesho Jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam amewekwa hadharani ambaye si mwingine ni Mathew Akrama kutoka mkoani Mwanza. Akrama anafahamika vema na vilabu hivyo kwani amewahi kuzihukumu misimu kadhaa iliyopita na amekuwa mkali awapo uwanjani, Akrama anakabidhiwa kipyenga wakati miamba hiyo itakapokutana kesho katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Awali jina la mwamuzi lilikuwa kizungumkuti na kuzua sintofahamu na baada ya TFF kuliweka hadharani jina hilo na kutuliza presha ya mashabiki wa vilabu hivyo, Akrama atasaidiwa na Mohamed Mkono na Hassan Zani

Ranieli atupiwa virago Leicester City

Picha
Bingwa mtetezi wa Ligi Kuu England Leicester City imemtimua Kocha wake mkuu, Muitaliano Claudio Ranieli, ikiwa ni miezi tisa baada ya kuiwezesha kupata ubingwa wa Ligi Kuu. Leicester iko katika nafasi ya 17, na ikipoteza alama moja tu italuwa kwenye mstari wa kushuka daraja, kutimuliwa kwa kocha huyo kumekuja saa 24 baada ya kichapo cha magoli 2-1 walichokipata kutoka kwa Sevilla. Leicester City msimu uliopita ilitwaa ubingwa kwa zaidi ya alama 10 mbele, lakini msimu huu mpaka sasa wamecheza michezo 25 ya ligi na kushinda mitano pekee, na imesalia michezo 13 ligi kuisha

Mavugo awa mwanasoka bora wa mwezi Januari Simba

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Klabu ya Simba wa mwezi Januari mwaka huu 2017. Huo ni mwanzo mzuri kwa straika huyo ambaye nyota yake imeanza kung' ara katika mechi tatu mfululizo zikiwemo mbili za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na moja ya kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu kombe la FA. Mavugo alifunga mfululizo kwenye mechi dhidi ya Majimaji ya Songea iliyofanyika mjini Songea Simba ikishinda 3-0 na nyingine alitupia dhidi ya Tanzania Prisons, Simba ikishinda 2-0 mechi ikipigwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Mshambuliaji huyo alifunga tena wakati Simba ikiifunga African Lyon bao 1-0 uwanja wa Taifa mchezo wa Kombe la FA, kwa maana hiyo anatunukiwa tuzo hiyo kubwa katika Klabu hiyo itakayomfanya aambulie kitita cha shilingi 500,000 inayotolewa na Klabu hiyo, Mavugo kwa sasa yupo Zanzibar na kikosi cha Simba ambacho kimeweka kambi kujiandaa na Yanga siku ya Jumamosi watakapokuta...

Makala: Chakori ni funzo kwa wasanii wetu, wabadilike

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Wasanii Mhe Nape Moses Nnauye majuzi alipiga marufuku uingizwaji na usambazwaji wa filamu za kigeni kwa vile zinaua soko la filamu za ndani. Hii yote imetokea baada ya filamu za Kitanzania maarufu Bongomovie kukosa soko, Wapenzi wa filamu nchini hawanunui tena filamu za hapa na wamekuwa wakitazama filamu za kigeni. Kwa maana hiyo wasanii wetu nchini wanakosa pesa za kuendesha maisha yao na kujikuta wakijitumbukiza kwenye skendo, hakuna mtu anayemfuatilia JB, Ray au Wema Sepetu, wala hakuna mtu anayemfuafilia Jengua, Irene Uwoya wala Johari, kwa kifupi wasanii wetu wamepoteza mvuto wa kibiashara tangu alipotutoka Steven Kanumba. Waziri Nape mbali ya kuzipiga stop filamu za nje, pia aliwataka wale wafanyabiashara wa maeneo ya Kariakoo hasa mitaa ya Agrey, Kongo na Msimbazi ambako ndiko inakofanyika biashara ya usambazaji wa filamu hizo kuacha mara moja mpaka pale utaratibu utakapopangwa. Inasemekana filamu za nje ...

Yanga wanasema wao wako vizuri kuliko Simba

Picha
Na Ikram Khamees. Kigamboni Baadhi ya wachezaji wa Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Yanga SC wameiambia Mambo Uwanjani kuwa wao wako vizuri kuliko watani zao Simba SC watakaokutana nao Jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba na Yanga zinakutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na zikiwa zimepita siku kadhaa tangu zikutane katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi kule Zanzibar ambapo Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90. Mshambuliaji wa Yanga raia wa Burundi Amissi Tambwe amesema Simba ni timu ya kawaida na haoni ubora wa kuizidi Yanga kwenye mchezo huo, Tambwe amedai Yanga ina kikosi kipana kuliko Simba na kingine kinachowapa jeuri na safu yao ya ushambuliaji. Nahodha Nadir Haroub "Cannavaro" yeye amekisifu kikosi cha Yanga na kudai kuwa safu ya ulinzi ya Yanga nayo ni imara kwani hadi sasa imeruhusu magoli tisa tu, Cannavaro ameongeza kuwa katika mchezo huo wao ndio watautaw...

Kaseja mchezaji bora Januari

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Golikipa wa timu ya Kagera Sugar, Juma Kaseja amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wa mwezi Januari kwa msimu wa 2016/2017. Kaseja aliwashinda wachezaji Mbaraka Yusuph pia wa Kagera Sugar na Jamal Mtengeta wa Toto Africans. Katika mechi tatu ambazo timu ya Kagera ilicheza kwa mwezi huo, Kaseja ambaye alicheza kwa dakika zote 270 alikuwa kiongozi na mhimili wa timu na aliisaidia timu yake kupata ushindi katiks michezo yote ambapo ilikusanya jumla ya pointi 9 zilizoifanya timu hiyo kupanda nafasi mbili katika msimamo wa ligi kwa mwezi huo wa Januari kutoka nafasi ya 5 hadi ya 3. Katika michezo hiyo mitatu Kagera Sugar ilifunga mabao sita na Kaseja alifungwa bao moja tu na alionyesha nidhamu ya hali ya juu ikiwemo kutopata onyo lolote (Kadi). Kwa kushinda tuzo hiyo Kaseja atazawadiwa kitita cha sh 1,000,000 (Milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo Kampuni ya Vodacom Tanzania

Yanga mbioni kuingia mkataba mnono na Tigo

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Dar Young Africans SC maarufu Yanga iko mbioni kuingia mkataba mnono wa udhamini na kampuni ya simu za kiganjani ya Tigo imefahamika. Taarifa ambazo Mambo Uwanjani inazo ni kwamba Tigo wataingia makubaliano na Yanga na huenda kampuni hiyo ikamwaga Shilingi Bilioni 4 kama sehemu ya udhamini huo ambao utaifanya Yanga kuwa Klabu kubwa barani Afrika. Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji aliwaambia Wanayanga kuwa Tigo wataidhamini Yanga hivi karibuni ili angalau Klabu ijiendeshe kimaslahi, Manji pia ndiye mmiliki wa Tigo aliyeinunua kampuni hiyo tangu mwaka 2014 licha ya kuwepo kesi mahakamani ikitaka mauzo yarudiwe tena baada ya kuwepo ubabaishaji. "Kwa sasa Manji ana matatizo, ngoja yaishe kwanza ndio tutazungumzia", alisema mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji wa Yanga, Manji amelazwa chini ya ulinzi wa polisi wa idara ya Uhamiaji katika hospitali ya Muhimbili Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete

Mourinho aipa ubingwa Chelsea

Picha
Meneja mtukutu wa Manchester United Jose Mourinho amekubali yaishe kwa vinara wa Ligi Kuu ya Primia maarufu EPL, Chelsea kwamba watabeba kikombe msimu huu huku akiiondoa timu yake kwenye mbio hizo. Mourinho amesema nafasi pekee iliyosalia kwa timu yake ni kushinda kombe la FA ambapo mchezo uliombele yao ni dhidi ya Chelsea, Mreno huyo mwenye rekodi ya aina yake amemsifu meneja wa Chelsea Antoine Conte. "Chelsea ndio mabingwa wa EPL hilo halina ubishi najipanga kuipa taji la FA, Man U", amesema Mourinho, mpaka sasa Man U inapigania kuingia kwenye Big Four na bado ipo nafasi ya sita

Rage awaambia Simba wenzake, waendelee kumuombea Ngoma asipone

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba, Alhaj Ismail Aden Rage ametoa utabiri wake wa pambano la watani wa jadi Simba na Yanga na kusema miamba hiyo itatoka sare katika mchezo huo. Rage sliyasema hayo leo asubuhi alipozungumza na kituo kimoja cha redio, Rage amedai mechi ya Simba na Yanga itakuwa ngumu na ya ushindani wa aina yake lakini mwisho wa siku miamba hiyo haitaamua mshindi na zitatoka sare iwe ya kufungana au suluhu. Ameongeza mwenyekiti huyo wa zamani ambaye pia aliwahi kuwa mchezaji wa Klabu hiyo miaka ya 60 na 70, kuwa Simba itaingia katika mchezo huo ikijivunia mabeki wake wa kati ambao hadi sasa wameruhusu magoli saba, wakati Yanga wao wanajivunia safu yao kali ya ushambuliaji. Rage pia amewataka wapenzi na mashabiki wa Simba kuendelea kumuomba Mungu ili mshambuliaji wa Yanga Mzimbabwe Donald Ngoma asipone haraka, Rage anaamini Ngoma akicheza dhidi ya Simba itakuwa balaa kwani anaijua shughuri yake awapo uwanjani

Mchezaji bora Afcon anunuliwa China

Picha
Kiungo wa kati wa Cameroon Christian Bassagog amejiunga na Klabu ya China ya Henan Jlanye, inayoshiriki michuano ya ligi kuu ya China kutoka klabu ya Aab Fodhold. Mapema mwezi huu mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alitajwa kuwa mchezaji bora wa Afcon baada ya Cameroon kupata ushindi wao wa tano kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon. Aab imemuuza Bassagog kwa klabu ya Henan Jlanye FC kwa rekodi ya uhamisho kuelekea Aab, klabu hiyo imesema katika taarifa yake, hata hivyo Bassagog alisema angeweza kulikataa pendekezo la yeye kutua China. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon alishiriki mechi zote sita katika Kombe la Mataifa, na kufunga bao katika hatua ya nusu fainali pale Indomitable Lions walipowachapa Ghana 2-0. Kwa sasa anakuwa miongoni mwa wachezaji wa Kiafrika kuelekea China, baada ya mchezaji wa Nigeria John Mikel Obi na Odion Ighalo walipojiunga na Tiajin Teda na Changchun Yatai mwezi uliopita

NGOMA BASI TENA YANGA

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Mshambuliaji wa kimataifa wa mabingwa wa soka nchini Yanga SC, Donald Dombo Ngoma ambaye ni raia wa Zimbabwe unaweza kusema basi tena, kwani anaendelea kuugua na huenda akaukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba. Mchezaji huyo tegemeo ameandamwa na majeruhi tangu mwishoni mwaka jana lakini alirejea kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand United Yanga ikishinda mabao 4-0 huku yeye akifunga bao la kwanza, kwa bahati mbaya Ngoma aliumia (Kama anavyoonekana pichani). Tangu alipoumia, Ngoma hakuweza kurejea uwanjani licha ya timu yake kufuzu raundi ya kwanza ya Ligi ya mabingwa barani Afrika pasipo huduma yake, Yanga ilisonga hatua hiyo baada ya kuifunga Ngaya Club ya Comoro mabao 6-2, ikishinda ugenini 5-1 kabla ya kulazimishwa sare nyumbani ya 1-1. Yanga itacheza na Simba Jumamosi ijayo na kwa mujibu wa Daktari wa Yanga Edward Bavu, Yanga itamkosa Ngoma ambaye bado anachechemea licha ya kuanza mazoezi mepesi, kikosi cha Yanga kimepiga kambi...

Ezekiel Kamwaga ajitokeza kujenga msikiti Tanga

Picha
Na Mwandishj Wetu. Dar es Salaam Aliyekuwa Afisa Habari wa zamani wa Klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga amejitokeza kusaidia ujenzi wa msikiti wa Waislamu huko mkoani Tanga. Akiandika kwenye ukurasa wa facebook, Kamwaga amesema ameamua kujenga msikiti kwa sababu Waislamu ni watu waungwana sana kwake na wala haoni shida kuungana nao. Kamwaga ambaye pia amewahi kuwa katibu mkuu wakati wa utawala wa Ismail Aden Rage amewataka rafiki zake ambao ni Waislamu kumsaidia vifaa vya ujenzi kwani ataianza kazi hiyo sasa, Kamwaga anaungwa mkono na watu kwakuonyesha mapenzi makubwa kwa waumizi wa dini hiyo ikiwa yeye ni Mkristo

YANGA YABANWA NA NGAYA, LAKINI YAPETA

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara Yanga SC jioni ya leo imeshindwa kuutumia uwanja wake wa nyumbani vizuri baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Ngaya Club de Mde ya Comoro katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Vijana wa Ngaya walicheza vizuri na kuonekana kuwamudu vilivyo Yanga ambao leo haikuwatumia nyota wake tegemeo kama Amissi Tambwe na Donald Ngoma, Ngaya waliandika bao la kuongoza mapema kabisa kipindi cha kwanza dakika ya 19 likifungwa na Zahir Mohamed aliyefumua shuti lililomgonga kichwani beki wa Yanga Vincent Bossou na kujaa wavuni. Yanga nao walijikakamua kutaka kusawazisha lakini washambuliaji wake wakiongozwa na Obrey Chirwa hawakuwa makini na kukosa nafasi za wazi, lakini walifanikiwa kusawazisha bao hilo kupitia beki wake wa kushoto Hajji Mwinyi Mngwali kwa shuti la mbali. Yanga sasa wametinga raundi ya kwanza Ligi ya Mabingwa barani Afrika na watakutana na Zanaco ya Zambia ambao leo wameishinda APR 1-0 nyumbani kwao Rwanda ...

Ney wa Mitego amzimia Diamond, asema Kiba bado sana

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Emmanuel Elibarik au Ney wa Mitego amesema msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinum' ni bora kuliko mwenzake Ally Kiba ambaye amekuwa akibebwa tu. Akizungumza na kituo kimoja cha televisheni hivi karibuni, Ney alisema Diamond ndiye mwanamuziki bora na anastahili vyote kwakuwa amekuwa akijitahidi kuitangaza Tanzania kimataifa na hata ufanisi wake mkubwa. "Diamond anajua kuimba, kuandika mashairi, kupangilia sauti na ala pia anajua kucheza na jukwaa, hata video zake ni nzuri tofauti na Ally Kiba ambaye watu tu wanaomchukia Diamond ndio wanaomtukuza Kiba, si kwamba Kiba ni mbaya sana ila hamuwezi Diamond", alisema Ney wa Mitego

Wenger kama Mugabe asema atafia Arsenal

Picha
Licha ya kipigo cha mabao 5-1 ilichokipata Arsenal toka kwa Buyern Munich ya Ujerumani katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, bado mkufunzi wa timu hiyo Arsenel Wenger ameendelea kusisitiza kuwa ataendelea kuiongoza Arsenal. Wenger amesema hatma yake ya kuondoka kwenye timu hiyo itategemea msimamo wake wa mwezi Machi au Aprili ambao utaamua kama aendelee kubaki Arsenal au kujiunga na timu nyingine, kwa maana hiyo Wenger anakuwa kama Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ambaye ametangaza tena kuwania Urais. Mugabe amesema ataendelea kuiongoza Zimbabwe hadi kifo kimkute, Wenger yuko katika shinikizo la kuondoka Arsenal kutokana na matokeo mabaya ya timu hiyo huku ikiwa haijatwaa ubingwa wa EPL tangu 2004, hivi karibuni mashabiki walibeba mabango yakimtaka aondoke

Yanga wasema wataifumua vibaya Ngaya kwa sababu ya jezi nyekundu

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Yanga SC wametamba kuifumua vibaya Ngaya Club iliyotua jana tayari kurudiana na Yanga Jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema vijana wake tayari kwa mchezo huo na wanahitaji kupata ushindi mnono ili kuandika rekodi, "Hatuangalii tunacheza na nani, tunataka ushindi tena mkubwa na vijana wamenipa matumaini", alisema Mwambusi. Nao mashabiki wa Yanga wamesema timu yao itapata ushindi mkubwa kwavile wapinzani wao (Ngaya) wanavaa jezi nyekundu na wameapa kuifunga magoli mengi ili kupeleka salamu kwa Wekundu wa Msimbazi ambao watakutana nao Februali 25 mwaka huu. Yanga ilishinda mabao 5-1 katika mchezo wa kwanza uliopigwa katika dimba la Bomel mjini Moroni nchini Comoro juma lililopita, katika mchezo wa kesho Yanga inahitaji sare yoyote ama kufungwa magoli matatu ilj wasonge raundi ya kwanza na wanaweza kucheza na APR au Zanaco. Nalo Shirikisho la s...

Kikwete kujenga uwanja wa kisasa Chalinze

Picha
Na Shaaban Hussein. Bagamoyo Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete kwa kushirikiana na kampuni ya Ujenzi ya nchini China wamekubaliana kujenga Uwanja wa kisasa maeneo ya Msoga Chalinze mkoani Pwani. Akizungumza juzi, Kikwete ambaye ni mtoto wa Rais wa Awamu ya nne ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amesema ujenzi huo wa uwanja utatumika kwa ajili ya mchezo wa soka na michezo mingineyo. Ameongeza kuwa hiyo ni ahadi yake kwa wapiga kura wa jimbo hilo kuwa atawajengea uwanja WanaChalinze, amedai tayari kampuni hiyo imeshaanza harakati za ujenzi na unaweza kukamilika kwa ajili ya mazoezi na hatua nyingine ya uwekaji uzio na majukwaa itafuata. "Hii ni fulsa kwa wakazi wa Chalinze kwani nimepania kuendeleza michezo kwenye jimbo langu, najua michezo ni ajira hivyo nimeona vema nianze mapema mchakato wa kujenga uwanja, nimeamua kuujenga Msoga ambapo ni nyumbani kwetu lengo ni kuinua michezo", Alisema.

Kiungo Yanga afariki dunia

Picha
Na Exipeditor Mataruma. Mbeya Kiungo wa zamani wa Yanga, Godfrey Bonny "Ndanje" amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu. Bonny maarufu kama Ndanje amefariki sunia baada ya kulazwa kwa muda mrefu katika Hospitalu ya Makandana, Tukuyu mkoani Mbeya. Nahodha wa zamani wa Yanga, Shadrack Nsajigwa "Fuso" ambayw alikuwa nahodha wakati Bonny akiichezea Yanga, amethibitisha taarifa hizo pamoja na dada wa marehemu. "Kweli nimepokea taarifa hizi za masikitiko, ndugu yetu ametangulia mbele za haki, Juhudi zilifanyika lakini Mungu alishapanga yake", alisema. Kiungo huyo aliichezea Yanga kwa kiwango kikubwa akitokea Tanzania Prisons ya jijini Mbeya. Baada ya kuondoka Yanga alikwenda nchini Nepal ambapo alicheza soka la kulipwa akiwa na Watanzania wengine akiwemo Nsajigwa na Pius Kisambale

MANJI AREJEA URAIANI, ATAKUWEPO JUKWAANI YANGA IKIWAVAA NGAYA J.MOSI

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam . Mfanyabiashara na mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Mehbood Manji leo alipansishwa kizimbani akikabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya na kutolewa kwa dhamana ya shilingi Milioni 10. Manji alifikishwa mahakamani hapo kujibu shitaka la kutumia dawa za kulevya baada ya mkemia mkuu wa serikali kuthibitisha kuwa Manji anatumia. Hata hivyo kesi hiyo iliahirishwa hadi Machi 17 mwaka huu ambapo Manji atapandishwa tena kujibu mashitaka yanayomkabili, Katibu mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa ndiye aliyemwekea dhamana hiyo na kumfanya arejee uraiani. Kwa maana hiyo Manji atakuwepo jukwaani wakati Yanga itakaporudiana na Ngaya Club ya Comoro Jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Kiingilio cha chini katika mchezo huo ni shilingi 3000 tu

Simba yatinga robo fainali kwa kulipiza kisasi

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Goli lililofungwa na Mrundi Laudit Mavugo limetosha kuipa ushindi Simba SC wa bao 1-0 dhidi ya African Lyon na kutinga hatua ya robo fainali michuano ya Azam Sports Federation Cup au FA Cup katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. African Lyon ikicheza kwa kujilinda zaidi katika kipindi cha kwanza ilijikuta ikifungwa bao hilo lililowaondosha moja kwa moja kwenye michuano hiyo, ushindi wa Simba leo ni kama kulipiza kisasi baada ya kufungwa 1-0 zilipokutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa kwanza mwaka jana. Simba imetinga hatua ya robo fainali na sasa itaingia kwenye maandalizi ya mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya mahasimu wake Yanga Februali 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Kikosi cha Simba kinachonolewa na Mcameroon Joseph Omog kilionekana kutawala zaidi sehemu ya kiungo na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga isipokuwa washambuliaji wake hawakuwa makini, Laudit Mavugo anaonekana kuimarika kabisa kwani hili ni goli lake ...

Mtoto wa nyota wa zamani wa Simba awaangukia mashabiki

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Mtoto wa Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Simba, Ally Machela (Kwa sasa ni marehemu), Abdul Machela (Pichani) amewaomba mashabiki wa soka nchini kumsaidia vifaa vya michezo hasa viatu kwakuwa amekosa vitu hivyo kutokana na ukata. Akizungumza na Mambo Uwanjani hivi karibuni, Machela amesema ukata umepelekea kukosa viatu na kushindwa kushiriki mchezo huo ipasavyo licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kusakata kandanda kama ilivyokuwa kwa marehemu baba yake ambaye alitamba na Simba kwenye miaka ya 90. Mchezaji huyo ambaye naye ni kiungo mshambuliaji anasema kwa sasa anaishi na bibi yake na anadai marehemu baba yake aliacha mali kadhaa lakini yeye anasikia vimetumika na ndugu wa marehemu baba yake. Anaongeza kuwa bibi yake hana uwezo wa kumsaidia viatu na yeye bado hajaanza maisha ya kujitegemea hivyo kama kuna mtu ataguswa kumnunua viatu basi yu tayari kuwasiliana naye, Machela Jr ametaja namba zake za simu kuwa ni 0657929124 na atashukuru endapo atasaidiwa ...

Mkude arejeshwa Simba, kuwavaa Yanga

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Kiungo na nahodha wa Simba hatimaye amerejeshwa tena kikosini baada ya kuwa nje kwa siku kadhaa kufuatia kutofautiana na kocha mkuu wa Simba Mcameroon Joseph Omog. Mchezaji huyo alikosa mechi mbili za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Majimaji iliyopigwa mjini Songea Simba ikishinda 3-0 na Tanzania Prisons iliyofanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam Simba tena ikishinda 3-0. Hofu ilianza kutanda kuelekea mpambano wa watani mechi ambayo itachezwa Februali 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, viongozi wa Simba walikutana kuzungumzia mchezo huo lakini wakaona umuhimu wa Mkude kwenye mchezo huo. Hivyo wakaamua kumrejesha na huenda akawemo kwenye mchezo huo muhimu utakaotoa sura ya ubingwa wa Bara, hata hivyo mchezaji huyo ameridhia kurejea kikosini na kuondoa uvumi kuwa abataka kujiunga na Yanga mwishoni mwa msimu

Masogange naye akamatwa

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya, Agnes Masogange (Pichani) amekanmatwa leo na kuunganishwa katika orodha ya watu wanaotajwa kutumia na kueneza madawa ya kulevya nchini. Masogange ambaye aliwahi kukamatwa nchini Afrika Kusini na madawa ya kulevya, alituhumiwa vikali na msanii mwenzake Wema Sepetu kuwa anahusika katika kashfa ya madawa ya kulevya na kwanini hakujumuhishwa katika orodha ya kwanza iliyotangazwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Poul Makonda. Wema na wenzake akina Mr Blue, Nyandu Toz, Chid Benz, T.I.D na wengineo walitajwa kuhusika na madawa ya kulevya, lakini baadaye ikadaiwa mkuu wa mkoa Poul Makonda alishindwa kumtaja Agnes Masogange kwakuwa na mchumba wake na amempangia nyumba Makongo

Ancelotti amkubali kinoma Wenger

Picha
Mkufubzi wa Bayern Munich, Carlo Ancelotti amemsifu mkufunzi mwenzake wa Arsenal Arsene Wenger kuwa anapaswa kupewa muda kuendelea kusalia kwenye kikosi hicho kwakuwa tayari amekiongoza katika mwanzo mzuri. Mashabiki wa Arsenal wakiwa na hasira walishika mabango yao walitaka Wenger aondoke kwenye timu hiyo kwakushinda kuwapa mafanikio kwa kipindi kirefu, Arsenal walichukua kikombe cha Primia mwaka 2004 hivyo mashabiki hawaoni kitu kipya cha Mfaransa huyo. Lakini Ancelotti ambaye amewahi kukinoa kikosi cha Chelsea, amedai Wenger ni mkufunzi bora kwa Arsenal kwani ameweza kuiweka timu hiyo kwenye nafasi za juu na pia kikosi hicho kimekuwa kikicheza vizuri, Arsenal na Bayern zilikutana katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya

African Lyon yaapa kuendeleza kisago kwa Simba kesho

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Timu ya soka ya African Lyon ya jijini Dar es Salaam imeapa kesho kuendeleza kipigo kwa vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara watakapokutana katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam mchezo wa kombe la Azam Sports Federation. Nahodha wa African Lyon, Hassan Isihaka, ameiambia Mambo Uwanjani leo kuwa Lyon kesho lazima wachomoze na ushindi kama walivyofanya katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara. "Simba ni timu ya kawaida sana na wala hatuoni sababu ya kushindwa kuifunga, tumewaona kwenye michezo waliyocheza na timu nyingine, wanafungika na sisi tuna dawa yao", alisema Isihaka ambaye aliwahi kuichezea Simba msimu uliopita

Makala: Tumuunge mkono Makonda vita ya madawa ya kulevya

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam VITA ya kupambana na madawa ya kulevya imeshaanza na watu mbalimbalj wametajwa kuhusishwa, hatua zimeanza kuchukuliwa na wahusika wameanza kufikishwa mahakamani na wengine bado wanaendelea kuchunguzwa. Madawa ya kulevya yameua nguvu kazi na kusababisha baadhi yao kuathilika, kwenye upande wa michezo ndio usiseme, vijana wengi wameathiliwa na dawa hizo, kwenye upande wa sanaa pia ni hivyo hivyo, kwa kifupi vijana wanateketea. Hakukuwa na jitihada zozote za kukabiliana na wafanyabiashara wakubwa wanaoziingiza kutoka Ughaibuni, vilevile hakukuwa na jitihada zozote kuwadhibiti wafanyabiashara wanaosambaza hapa nchini. Vijana wanazidi kuzitumia na kujikuta wakipoteza nguvu zao ambazo ziljwafanya waweze kujirafutia riziki na baadaye kujikuta hawana nguvu kabisa na kujiingiza kwenye uporaji, makundi ya vijana waliojiingiza kwenye matumizi ya mihadarati wengi wao waporaji. Na wanafanya hivyo kwakuwa hawana uwezo wa kufanya kazi ambazo ziliwafanya wajipatie pe...

MANJI ABADILISHIWA SHITAKA, SASA KUFIKISHWA MAHAKAMANI

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Jeshi la polisi idara ya Uhamiaji limemkuta na hatia Mkurugenzi wa kampuni ya Quality Group na mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Yusuf Manji ya kuwaajili kwenye kampuni yake wafanyakazi wanaoishi nchini na sheria. Uhamiaji imesema itamfikisha mahakamanj Mkurugenzi huyo na wafanyakazi wake hao ambao waligundulika hivi karibuni wakati jeshi la polisi lilipokwenda kufanya ukaguzi kwenye kampuni hiyo iliyopo pembezoni mwa barabara ya Nyerere. Ukaguzi huo ulifanyika baada ya Manji kutajwa katika listi ya watu 65 ya washukiwa wa madawa ya kulevya ambapo yeye na Mchungaji Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo waliwahi Alhamisi badala ya Ijumaa siku ambayo walitakiwa kuhojiwa na polisi katika kituo cha kati (Central). Hata hivyo Manji na Gwajima walishikiliwa kwa siku tatu kabla ya kuachiwa lakini Manji alipelekwa hospitali baada ya kuugua ghafla, Uhamiaji itamfikisha mahakamani mara baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali ambako inadaiwa amelazwa

Yule kinda wa Serengeti Boys aliywfuzu Tunisia kuanza kukinukisha baada ya Afcon

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Kiungo mshambuliaji kinda wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys Yohana Mkomola ambaye hivi karibuni alikuwa ajifanya majaribio ya kutaka kucheza soka la kulipwa katika Klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia na kufaulu sasa ataichezea timu hiyo baada ya kukamilika kwa Afcon ya vijana wenye umri huo zitakazofanyika Gabon. Mambo Uwanjani imedokezwa kuwa Mkomola atajiunga na Etoile mara baada ya kumalizika michuano ya mataifa ya Afrika kwa vijana wenye miaka 17 inayotarajia kuanza hivi karibuni nchini Gabon, Mkomola alifaulu majaribio yake kwenye Klabu hiyo kongwe barani Afrika hivyo sasa atakuwa Mtanzania mwingine anayecheza soka la kulipwa baada ya akina Mbwana Samatta anayecheza Ubelgiji, Thomas Ulimwengu Sweden na Farid Mussa Hispania. Mkomola alikuwa mmoja kati ya nyota wa Serengeti Boys walioiwezesha timu hiyo kufuzu fainali za michuano hiyo, nyota huyo alifunga magoli mawili wakati Serengeti ikiifunga Congo Brazaville ...

Conte akasirishwa na maneno ya Mourinho

Picha
Meneja wa Chelsea Antoine Conte ameonyesha kukasirishwa na maneno ya meneja wa Manchester United Jose Mourinho na kusema yeye hapendi mzaha mzaha. Mourinho amesikika akisema kuwa Chelsea inacheza kwa kujilinda zaidi na ndio maana ilitoshana nguvu na Burnley ya kufungana 1-1 ikiongoza Ligi ya Primia kwa tofauti ya pointi 10. Conte amedai Mourinho amekuwa akipenda mzaha na hasa baada ya timu yake ya Man U kushinda 2-0 dhidi ya Watford, Mourinho amewahi kuiongoza Chelsea

Kaburu asema bila kuifunga Yanga ubingwa hauwezekani Msimbazi

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba Geofrey Nyange Hiliki "Kaburu" ameuzungumzia ubingwa wa Tanzania Bara kuwa ili Simba iweze kuunyakua lazima aifunge Yanga ama sivyo utabakia historia kwao. Kaburu amesema Yanga wanaiheshimu lakini wataifunga katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara utakaofanyika Februali 25 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Akizungumza leo, Kaburu amedai kikosi cha Simba kitaibuka na ushindi katika mchezo huo kwani wanaifahamu vizuri Yanga na wataifunga, "Tuliifunga Yanga kwa mikwaju ya penalti kule Zanzibar kakini tunataka kuwafunga ndani ya dakika 90", alisema Kaburu