Kaburu asema bila kuifunga Yanga ubingwa hauwezekani Msimbazi
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba Geofrey Nyange Hiliki "Kaburu" ameuzungumzia ubingwa wa Tanzania Bara kuwa ili Simba iweze kuunyakua lazima aifunge Yanga ama sivyo utabakia historia kwao.
Kaburu amesema Yanga wanaiheshimu lakini wataifunga katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara utakaofanyika Februali 25 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Akizungumza leo, Kaburu amedai kikosi cha Simba kitaibuka na ushindi katika mchezo huo kwani wanaifahamu vizuri Yanga na wataifunga, "Tuliifunga Yanga kwa mikwaju ya penalti kule Zanzibar kakini tunataka kuwafunga ndani ya dakika 90", alisema Kaburu