Yanga waapa kula sahani moja na Simba kileleni, kuvaana na Ruvu, J,tano

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajia kuendelea tena Jumatano ijayo ambapo mabingwa watetezi wa taji hilo, Yanga SC itawaalika Ruvu Shooting kwenye mchezo utakaofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Yanga wameapa kuifukuzia Simba kileleni na wameahidi kushinda mchezo huo ili kuwapoza mashabiki wake baada ya Jumamosi iliyopita kufungwa 2-1 na Simba, mbali na mchezo huo mmoja wa Jumatano, ligi hiyo itaendelea siku ya Jumamosi Machi 4 mwaka huu Simba itacheza na Mbeya City Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Ukiacha mchezo huo, michezo mingine ya Jumamosi Machi 4, mwaka huu itakuwa ni kati ya Toto Africans na Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, huku Kagera Sugar ikiikaribisha Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Azam FC pia itacheza na Stand United ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Chamazi, Mchezo huo utaanza saa 1:00 jioni wakati mechi nyingine zitaanza saa 10:00 jioni.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeirejesha tena mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Mtibwa Sugar na Yanga SC sasa mechi hiyo itapigwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, mechi hiyo ingechezwa Dar es Salaam hasa baada ya TFF kuufungia uwanja huo.

Mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utachezwa Uwanja wa Uhuru ambako African Lyon itaialika Mwadui ya Shinyanga wakati Ndanda FC itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA