Kamusoko atajwa kipigo cha Yanga jana
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Baada ya Yanga SC kuchapwa mabao 2-1 na hasimu wake mkuu Simba SC jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara takwimu mbalimbali zimetolewa na wataalamu wa mambo ya soka.
Juma Mwambusi ambaye ni kocha msaidizi wa Yanga ametoboa kilichoiua Yanga jana kuwa ni kuumia kwa kiungo wake Mzimbabwe Thabani Kamusoko, Kocha huyo wa zamani wa Tanzania Prisons na Mbeya City zote za mkoani Mbeya amedai Kamusoko ndiye aliyewadhibiti mno viungo wa Simba.
"Kwakweli jana tumepotea pale alipotoka Kamusoko baada ya kuumia, nina hakika kama asingetoka kwa kuumia basi kipindi cha pili tungeendelea kuutawala mchezo na tungeshinda", anasema Mwambusi alipohojiwa na Mambo Uwanjani leo kuelezea mchezo wa jana.
Yanga wanajipanga kwa mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa Jumatano ijayo kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam ukiwa ni mchezo wake uliosalia mkononi ili kutimiza mechi 23 sawa na vinara wa ligi hiyo Simba