Mkwasa asema Yanga haina fedha kwa sasa

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Katibu mkuu wa Yanga SC Charles Boniface Mkwasa amefunguka mazito na kudai sababu ya kuboronga kwa kikosi chake kilipocheza na Simba na kufungwa mabao 2-1 juzi katika Uwanja wa Taifa jijinj Dar es Salaam.

Mkwasa ambaye kitaaluma ni kocha, amesema Yanga ina matatizo ya kifedha kwa sasa hasa baada ya mwenyekiti wake Yusuf Manji kuandamwa na misukosuko na serikali na kupelekea kufungwa kwa akaunti zake zote.

Licha ya kufungwa kwa akaunti hizo za Manji ambaye pia ni mfadhili wa timu hiyo, Mkwasa amedai Yanga haitashindwa kumudu gharama za kambi na usafiri na wamejidhatiti kutetea ubingwa wao wa Bara.

Yanga ilikubali kichapo cha mabao 2-1 toka kwa mahasimu wao Simba Jumamosi iliyopita kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Yanga ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na Simon Msuva kwa penalti dakika ya sita kipindi cha kwanza.

Simba walisawazisha kupitia kwa Laudit Mavugo na kuongeza la ushindi kupitia kwa Shiza Kichuya, hata hivyo Simba waliweza kucheza wakiwa pungufu baada ya beki wake Mkongoman Janviel Bokungu kulambishwa kadi nyekundu

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA