Ney wa Mitego amzimia Diamond, asema Kiba bado sana
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Emmanuel Elibarik au Ney wa Mitego amesema msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinum' ni bora kuliko mwenzake Ally Kiba ambaye amekuwa akibebwa tu.
Akizungumza na kituo kimoja cha televisheni hivi karibuni, Ney alisema Diamond ndiye mwanamuziki bora na anastahili vyote kwakuwa amekuwa akijitahidi kuitangaza Tanzania kimataifa na hata ufanisi wake mkubwa.
"Diamond anajua kuimba, kuandika mashairi, kupangilia sauti na ala pia anajua kucheza na jukwaa, hata video zake ni nzuri tofauti na Ally Kiba ambaye watu tu wanaomchukia Diamond ndio wanaomtukuza Kiba, si kwamba Kiba ni mbaya sana ila hamuwezi Diamond", alisema Ney wa Mitego