Mtoto wa nyota wa zamani wa Simba awaangukia mashabiki
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Mtoto wa Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Simba, Ally Machela (Kwa sasa ni marehemu), Abdul Machela (Pichani) amewaomba mashabiki wa soka nchini kumsaidia vifaa vya michezo hasa viatu kwakuwa amekosa vitu hivyo kutokana na ukata.
Akizungumza na Mambo Uwanjani hivi karibuni, Machela amesema ukata umepelekea kukosa viatu na kushindwa kushiriki mchezo huo ipasavyo licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kusakata kandanda kama ilivyokuwa kwa marehemu baba yake ambaye alitamba na Simba kwenye miaka ya 90.
Mchezaji huyo ambaye naye ni kiungo mshambuliaji anasema kwa sasa anaishi na bibi yake na anadai marehemu baba yake aliacha mali kadhaa lakini yeye anasikia vimetumika na ndugu wa marehemu baba yake.
Anaongeza kuwa bibi yake hana uwezo wa kumsaidia viatu na yeye bado hajaanza maisha ya kujitegemea hivyo kama kuna mtu ataguswa kumnunua viatu basi yu tayari kuwasiliana naye, Machela Jr ametaja namba zake za simu kuwa ni 0657929124 na atashukuru endapo atasaidiwa