Bossou aigomea Yanga, kisa mshahara

Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam

Mlinzi wa kimataifa wa Togo, Vincent Bossou (Pichani) amegoma kukipiga Yanga akidai mshahara wake wa mwezi Januari, mlinzi huyo alimkatalia kocha Mzambia George Lwandamina kucheza dhidi ya Simba Jumamosi iliyopita katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Taarifa ambazo Mambo Uwanjani imezinyaka kuwa Bossou alikataa kucheza mechi hiyo dhidi ya Simba ambapo Yanga iliweza kulala 2-1, ukuta wa Yanga ulisimamiwa na :Mhandisi' Kevin Yondani na Vincent Andrew 'Dante' na ukaruhusu mabao hayo yaliyowekwa kimiani na Mrundi Laudit Mavugo na Shiza Kichuya.

Kwa maana hiyo Bossou atakosekana kwenye mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara ambapo Yanga itacheza na Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Bossou anaidai Yanga mshahara wa mwezi Januari na kwa mujibu wa Katibu mkuu wa Yanga Charles Mkwasa kuwa Bossou peke ndiyo hakulipwa Januari kwakuwa alikuwa nje ya nchi.

Bossou aliungana na timu ya taifa ya Togo ilikwenda kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika zilizofanyika Gabon mapema Januari, hata hivyo uwezekano wa kulipwa beki huyo ni mdogo kwakuwa mshahara wake uko Quality Group ambao akaunti zao zimefungwa na serikali

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA