Mchezaji bora Afcon anunuliwa China

Kiungo wa kati wa Cameroon Christian Bassagog amejiunga na Klabu ya China ya Henan Jlanye, inayoshiriki michuano ya ligi kuu ya China kutoka klabu ya Aab Fodhold.

Mapema mwezi huu mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alitajwa kuwa mchezaji bora wa Afcon baada ya Cameroon kupata ushindi wao wa tano kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon.

Aab imemuuza Bassagog kwa klabu ya Henan Jlanye FC kwa rekodi ya uhamisho kuelekea Aab, klabu hiyo imesema katika taarifa yake, hata hivyo Bassagog alisema angeweza kulikataa pendekezo la yeye kutua China.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon alishiriki mechi zote sita katika Kombe la Mataifa, na kufunga bao katika hatua ya nusu fainali pale Indomitable Lions walipowachapa Ghana 2-0.

Kwa sasa anakuwa miongoni mwa wachezaji wa Kiafrika kuelekea China, baada ya mchezaji wa Nigeria John Mikel Obi na Odion Ighalo walipojiunga na Tiajin Teda na Changchun Yatai mwezi uliopita

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA