Mavugo awa mwanasoka bora wa mwezi Januari Simba

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Klabu ya Simba wa mwezi Januari mwaka huu 2017.

Huo ni mwanzo mzuri kwa straika huyo ambaye nyota yake imeanza kung' ara katika mechi tatu mfululizo zikiwemo mbili za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na moja ya kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu kombe la FA.

Mavugo alifunga mfululizo kwenye mechi dhidi ya Majimaji ya Songea iliyofanyika mjini Songea Simba ikishinda 3-0 na nyingine alitupia dhidi ya Tanzania Prisons, Simba ikishinda 2-0 mechi ikipigwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mshambuliaji huyo alifunga tena wakati Simba ikiifunga African Lyon bao 1-0 uwanja wa Taifa mchezo wa Kombe la FA, kwa maana hiyo anatunukiwa tuzo hiyo kubwa katika Klabu hiyo itakayomfanya aambulie kitita cha shilingi 500,000 inayotolewa na Klabu hiyo, Mavugo kwa sasa yupo Zanzibar na kikosi cha Simba ambacho kimeweka kambi kujiandaa na Yanga siku ya Jumamosi watakapokutana uwanja wa Taifa mchezo wa VPL

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA