Masogange naye akamatwa
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya, Agnes Masogange (Pichani) amekanmatwa leo na kuunganishwa katika orodha ya watu wanaotajwa kutumia na kueneza madawa ya kulevya nchini.
Masogange ambaye aliwahi kukamatwa nchini Afrika Kusini na madawa ya kulevya, alituhumiwa vikali na msanii mwenzake Wema Sepetu kuwa anahusika katika kashfa ya madawa ya kulevya na kwanini hakujumuhishwa katika orodha ya kwanza iliyotangazwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Poul Makonda.
Wema na wenzake akina Mr Blue, Nyandu Toz, Chid Benz, T.I.D na wengineo walitajwa kuhusika na madawa ya kulevya, lakini baadaye ikadaiwa mkuu wa mkoa Poul Makonda alishindwa kumtaja Agnes Masogange kwakuwa na mchumba wake na amempangia nyumba Makongo