Ancelotti amkubali kinoma Wenger

Mkufubzi wa Bayern Munich, Carlo Ancelotti amemsifu mkufunzi mwenzake wa Arsenal Arsene Wenger kuwa anapaswa kupewa muda kuendelea kusalia kwenye kikosi hicho kwakuwa tayari amekiongoza katika mwanzo mzuri.

Mashabiki wa Arsenal wakiwa na hasira walishika mabango yao walitaka Wenger aondoke kwenye timu hiyo kwakushinda kuwapa mafanikio kwa kipindi kirefu, Arsenal walichukua kikombe cha Primia mwaka 2004 hivyo mashabiki hawaoni kitu kipya cha Mfaransa huyo.

Lakini Ancelotti ambaye amewahi kukinoa kikosi cha Chelsea, amedai Wenger ni mkufunzi bora kwa Arsenal kwani ameweza kuiweka timu hiyo kwenye nafasi za juu na pia kikosi hicho kimekuwa kikicheza vizuri, Arsenal na Bayern zilikutana katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA