Bila ya Ranieli, Leicester yaifumua Liverpool 3-1

Leicester City wamejikokota na kupanda hadi nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya kuizaba Liverpool kwa mabao 3-1.

Leicester walionyesha kiwango cha juu na magoli mawili kutoka kwa Jamie Vardy na moja kutoka kwa Danny Drinkwater yaliididimiza Liverpool.

Wakicheza chini ya kaimu kocha Craig Shakespeare aliyechukua mikoba ya Claudio Ranieli, mabingwa hao wa England walicheza kama mabingwa watetezi.

Goli la kwanza la Jamie Vardy limekumbusha mtindo waliokuwa wakicheza msimu uliopita, baada ya pasi murua kutoka kwa Marc Aibrighton iliyomfikia Vardy. Magoli hayo ya Leicester ndio magoli ya kwanza kwa klabu hiyo kufunga mwaka huu wa 2017.

Liverpool ambao wangeweza kupanda hadi nafasi ya tatu iwapo wangepata ushindi, sasa wamepoteza mechi tano kati ya saba walizocheza katika michuano yote

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA