Messi aipeleka Azam robo fainali FA Cup
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Goli pekee lililofungwa na kiungo mshambuliaji Ramadhan Singano "Messi" lilitosha kabisa kuwaua Mtibwa Sugar na kuipeleka robo fainali Azam FC katika mchezo wa kombe la Azam Sports Federation Cup au maarufu FA Cup kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Mchezo ulikuwa mkali na wa aina yake kwa timu zote kuonyeshana upinzani ambapo Azam FC ilionekana kucheza vema kwa kipinsi kirefu kabla ya Mtibwa Sugar inayonolewa na mchezaji wake wa zamani Zuberi Katwila haijatawala dakika 20 za mwisho.
Azam ilianza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la mapema dakika ya 6 likifungwa na Messi ambaye aliwahi kuichezea Simba misimu miwili iliyopita, Messi aligongeana vema na Salum Abubakar "Sure Boy" ambaye aliendeleza kiwango kizuri katika mtanange huo.
Mabingwa hao wa Ngao ya Jamii na Kombe la Mapinduzi waliendeleza kasi yao ili kusaka mabao zaidi lakini safu ya ulinzi ya Mtibwa Sugar ilikuwa makini kumdhibiti mshambuliaji pekee aliyekuwa amesimamishwa mbele Yahaya Mohamed kila alupogusa mpira