Wenger kama Mugabe asema atafia Arsenal

Licha ya kipigo cha mabao 5-1 ilichokipata Arsenal toka kwa Buyern Munich ya Ujerumani katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, bado mkufunzi wa timu hiyo Arsenel Wenger ameendelea kusisitiza kuwa ataendelea kuiongoza Arsenal.

Wenger amesema hatma yake ya kuondoka kwenye timu hiyo itategemea msimamo wake wa mwezi Machi au Aprili ambao utaamua kama aendelee kubaki Arsenal au kujiunga na timu nyingine, kwa maana hiyo Wenger anakuwa kama Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ambaye ametangaza tena kuwania Urais.

Mugabe amesema ataendelea kuiongoza Zimbabwe hadi kifo kimkute, Wenger yuko katika shinikizo la kuondoka Arsenal kutokana na matokeo mabaya ya timu hiyo huku ikiwa haijatwaa ubingwa wa EPL tangu 2004, hivi karibuni mashabiki walibeba mabango yakimtaka aondoke

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA