Yule kinda wa Serengeti Boys aliywfuzu Tunisia kuanza kukinukisha baada ya Afcon
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Kiungo mshambuliaji kinda wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys Yohana Mkomola ambaye hivi karibuni alikuwa ajifanya majaribio ya kutaka kucheza soka la kulipwa katika Klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia na kufaulu sasa ataichezea timu hiyo baada ya kukamilika kwa Afcon ya vijana wenye umri huo zitakazofanyika Gabon.
Mambo Uwanjani imedokezwa kuwa Mkomola atajiunga na Etoile mara baada ya kumalizika michuano ya mataifa ya Afrika kwa vijana wenye miaka 17 inayotarajia kuanza hivi karibuni nchini Gabon, Mkomola alifaulu majaribio yake kwenye Klabu hiyo kongwe barani Afrika hivyo sasa atakuwa Mtanzania mwingine anayecheza soka la kulipwa baada ya akina Mbwana Samatta anayecheza Ubelgiji, Thomas Ulimwengu Sweden na Farid Mussa Hispania.
Mkomola alikuwa mmoja kati ya nyota wa Serengeti Boys walioiwezesha timu hiyo kufuzu fainali za michuano hiyo, nyota huyo alifunga magoli mawili wakati Serengeti ikiifunga Congo Brazaville mabao 3-2 katika mchezo wa kwanza uliofanyika uwanja wa Taifa Dar es Salaam kabla ya kwenda kulala 1-0 ugenini kisha kutolewa kabla ya CAF kuipa ushindi wa mezani baada ya Congo kumtumia mchezaji mwenye umri mkubwa