African Lyon yaapa kuendeleza kisago kwa Simba kesho
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Timu ya soka ya African Lyon ya jijini Dar es Salaam imeapa kesho kuendeleza kipigo kwa vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara watakapokutana katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam mchezo wa kombe la Azam Sports Federation.
Nahodha wa African Lyon, Hassan Isihaka, ameiambia Mambo Uwanjani leo kuwa Lyon kesho lazima wachomoze na ushindi kama walivyofanya katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara.
"Simba ni timu ya kawaida sana na wala hatuoni sababu ya kushindwa kuifunga, tumewaona kwenye michezo waliyocheza na timu nyingine, wanafungika na sisi tuna dawa yao", alisema Isihaka ambaye aliwahi kuichezea Simba msimu uliopita