Yanga wasema wataifumua vibaya Ngaya kwa sababu ya jezi nyekundu

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Yanga SC wametamba kuifumua vibaya Ngaya Club iliyotua jana tayari kurudiana na Yanga Jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema vijana wake tayari kwa mchezo huo na wanahitaji kupata ushindi mnono ili kuandika rekodi, "Hatuangalii tunacheza na nani, tunataka ushindi tena mkubwa na vijana wamenipa matumaini", alisema Mwambusi.

Nao mashabiki wa Yanga wamesema timu yao itapata ushindi mkubwa kwavile wapinzani wao (Ngaya) wanavaa jezi nyekundu na wameapa kuifunga magoli mengi ili kupeleka salamu kwa Wekundu wa Msimbazi ambao watakutana nao Februali 25 mwaka huu.

Yanga ilishinda mabao 5-1 katika mchezo wa kwanza uliopigwa katika dimba la Bomel mjini Moroni nchini Comoro juma lililopita, katika mchezo wa kesho Yanga inahitaji sare yoyote ama kufungwa magoli matatu ilj wasonge raundi ya kwanza na wanaweza kucheza na APR au Zanaco.

Nalo Shirikisho la soka nchini (TFF) limewaonya mashabiki wa Yanga kutobeba mabango yoyote ya kuikashifu serikali au kiongozi yeyote kutokana na kukamatwa kwa mwenyekiti wao Yusuf Manji hivi karibuni na kuachiwa kwa dhamana jana

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA