Simba yapeleka maafa Jangwani

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Simba SC jioni ya leo imefanikiwa kuilaza Yanga SC mabao 2-1 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Yanga walionekana kuutawala mchezo katika dakika 20 za mwanzo kipindi cha kwanza na waliandika bao la kuongoza lililofungwa na Simon Msuva kwa mkwaju wa penalti kufuatia Obrey Chirwa kukwatuliwa kwenye eneo la hatari.

Yanga waliendelea kuliandama lango la Simba lakini kocha wa Simba alifanya mabadiliko ya kumtoa Juma Luizio na kumwingiza Said Ndemla ambaye aliweza kuubadili mchezo na Simba kutakata, hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele.

Kipindi cha pili Simba walianza kwa spidi na kulitia msukomsuko lango la Yanga na kufanikiwa kusawazisha kupitia Mrundi Laudit Mavugo "King Loud" na kuongeza la pili lililofungwa na Shiza Kichuya.

Simba sasa wamefikisha pointi 54 wakiwa mbele kwa tofauti ya pointi tano na wapinzani wao Yanga ambao wana pointi 49 wakicheza mechi 22 wakati Simba wamecheza mechi 23, mwamuzi wa mchezo wa leo Mathew Akrama wa Mwanza alimpa kadi nyekundu Janviel Bokungu kwa kucheza rafu mbaya

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA