NGOMA BASI TENA YANGA
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Mshambuliaji wa kimataifa wa mabingwa wa soka nchini Yanga SC, Donald Dombo Ngoma ambaye ni raia wa Zimbabwe unaweza kusema basi tena, kwani anaendelea kuugua na huenda akaukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.
Mchezaji huyo tegemeo ameandamwa na majeruhi tangu mwishoni mwaka jana lakini alirejea kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand United Yanga ikishinda mabao 4-0 huku yeye akifunga bao la kwanza, kwa bahati mbaya Ngoma aliumia (Kama anavyoonekana pichani).
Tangu alipoumia, Ngoma hakuweza kurejea uwanjani licha ya timu yake kufuzu raundi ya kwanza ya Ligi ya mabingwa barani Afrika pasipo huduma yake, Yanga ilisonga hatua hiyo baada ya kuifunga Ngaya Club ya Comoro mabao 6-2, ikishinda ugenini 5-1 kabla ya kulazimishwa sare nyumbani ya 1-1.
Yanga itacheza na Simba Jumamosi ijayo na kwa mujibu wa Daktari wa Yanga Edward Bavu, Yanga itamkosa Ngoma ambaye bado anachechemea licha ya kuanza mazoezi mepesi, kikosi cha Yanga kimepiga kambi Kigamboni kwa ajili ya kuiwinda Simba