Pacquiao kuzichapa na Khan Aprili

Bingwa wa ndondi uzani wa WelterWeight duniani Manny Pacquiao, atapigana na Muingereza Amir Khan tarehe 23 Aprili mwaka huu.

Pambano hilo litaandaliwa baada ya mashabiki wa Pacquiao kwenye mtandao wa Twitter kumchagua Khan kama mwanamasumbwi ambaye wangependa apigane na Mfilipino huyo.

"Hiki ndicho mashabiki walikuwa wanataka", Pacquiao mwenye umri wa miaka 38 alisema. Khan wa umri wa miaka 30 alithibitisha pigano hilo licha ya Pacauiao kusema kuwa huenda pigano lake likaandaliwa katika miliki ya nchi za Kiarabu, eneo litakaliandaliwa bado halihatangazwa.

Akiongea kwa njia ya video Khan anasema Uingereza, Dubai au Marekani ni kati ya sehemu ambapo pambano hilo likafanyika.

Pigano la mwisho la Khan lilifanyika mwezi Mei mwaka 2016, wakati alimsginda kwa Knock out raia wa Mexico Saul "Canelo" Alvarez

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA