Ezekiel Kamwaga ajitokeza kujenga msikiti Tanga
Na Mwandishj Wetu. Dar es Salaam
Aliyekuwa Afisa Habari wa zamani wa Klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga amejitokeza kusaidia ujenzi wa msikiti wa Waislamu huko mkoani Tanga.
Akiandika kwenye ukurasa wa facebook, Kamwaga amesema ameamua kujenga msikiti kwa sababu Waislamu ni watu waungwana sana kwake na wala haoni shida kuungana nao.
Kamwaga ambaye pia amewahi kuwa katibu mkuu wakati wa utawala wa Ismail Aden Rage amewataka rafiki zake ambao ni Waislamu kumsaidia vifaa vya ujenzi kwani ataianza kazi hiyo sasa, Kamwaga anaungwa mkono na watu kwakuonyesha mapenzi makubwa kwa waumizi wa dini hiyo ikiwa yeye ni Mkristo