MANJI AREJEA URAIANI, ATAKUWEPO JUKWAANI YANGA IKIWAVAA NGAYA J.MOSI
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
.
Mfanyabiashara na mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Mehbood Manji leo alipansishwa kizimbani akikabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya na kutolewa kwa dhamana ya shilingi Milioni 10.
Manji alifikishwa mahakamani hapo kujibu shitaka la kutumia dawa za kulevya baada ya mkemia mkuu wa serikali kuthibitisha kuwa Manji anatumia.
Hata hivyo kesi hiyo iliahirishwa hadi Machi 17 mwaka huu ambapo Manji atapandishwa tena kujibu mashitaka yanayomkabili, Katibu mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa ndiye aliyemwekea dhamana hiyo na kumfanya arejee uraiani.
Kwa maana hiyo Manji atakuwepo jukwaani wakati Yanga itakaporudiana na Ngaya Club ya Comoro Jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Kiingilio cha chini katika mchezo huo ni shilingi 3000 tu