Ally Kiba, Diamond Platinumz waitwa kamati ya Serengeti Boys

Waziri wa Habari, Michezo, Utamaduni na Wasanii Nape Moses Nnauye ametangaza majina ya watu kumi kuunda kamati ya kuhamasisha ushiriki wa Tanzania katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ambapo Serengeti Boys itashiriki kwenye fainali hizo zitakazofanyika Gabon.

Katika uteuzi wake, Mhe Nape mbali ya kumteua Mwesigwa Celestine kuwa katibu wa kamati hiyo aliwateua wasanii wa muziki wa kizazi kipya Ally Kiba na Diamond Platinumz.

Wengine walioitwa kwenye kamati hiyo ni Beatrice Singano, Charles Hilaly, Eric Shigongo, Maulid Kitenge na wengineo ambao mbali na kusaidia uhamasishaji kwa timu hiyo ya Serengeti Boys ili iweze kupatiwa misaada mbalimbali ya kifedha ili ishiriki vema pia mjadala wa Tanzania kushiriki Olimpiki nao ulijadiliwa

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA