Manara amlilia Kessy Yanga
Na Shafih Matuwa. Dar es Salaam
Afisa Habari wa Klabu ya Simba Haji Sunday Manara amemsikitikia mlinzi wao wa zamani Hassan Ramadhan Kessy kwa kuendelea kusugua benchi kwenye kikosi cha Yanga hivi sasa na kushindwa kumshawishi kocha Mzambia George Lwandamina ili ampange.
Manara aliyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo alidai kuwa Kessy aliihama Simba kwa kebehi akilalamika kwamba Simba ilishindwa kumtimizia ahadi yake.
Mchezaji huyo alisajiliwa na Yanga kwa utata mkubwa kwani mkataba wake na Simba ulikuwa bado haujakwisha kitendo kilichozua sekeseke lililopelekea Simba kushitaki TFF ambapo Yanga walitakiwa kuilipa Simba shilingi Milioni 50.
Lakini maisha ya beki huyo ndani ya Yanga yanaonekana kama magumu kwani amekuwa akisoteshwa benchi kila mara huku Juma Abdul akicheza karibu mechi zote kuanzia kombe la Mapinduzi, Ligi Kuu Bara, kombe la FA na michuano ya kimataifa na Manara anasema Kessy atajuuta