YANGA YABANWA NA NGAYA, LAKINI YAPETA

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara Yanga SC jioni ya leo imeshindwa kuutumia uwanja wake wa nyumbani vizuri baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Ngaya Club de Mde ya Comoro katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Vijana wa Ngaya walicheza vizuri na kuonekana kuwamudu vilivyo Yanga ambao leo haikuwatumia nyota wake tegemeo kama Amissi Tambwe na Donald Ngoma, Ngaya waliandika bao la kuongoza mapema kabisa kipindi cha kwanza dakika ya 19 likifungwa na Zahir Mohamed aliyefumua shuti lililomgonga kichwani beki wa Yanga Vincent Bossou na kujaa wavuni.

Yanga nao walijikakamua kutaka kusawazisha lakini washambuliaji wake wakiongozwa na Obrey Chirwa hawakuwa makini na kukosa nafasi za wazi, lakini walifanikiwa kusawazisha bao hilo kupitia beki wake wa kushoto Hajji Mwinyi Mngwali kwa shuti la mbali.

Yanga sasa wametinga raundi ya kwanza Ligi ya Mabingwa barani Afrika na watakutana na Zanaco ya Zambia ambao leo wameishinda APR 1-0 nyumbani kwao Rwanda

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA