Asiye na mwana abebe jiwe, Simba vs Yanga

Na Prince Hoza. Dar es Salaam

Wafalme wa soka nchini Simba na Yanga wanakutana jioni ya leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Maneno mengi yamesemwa hasa kutoka kwenye vijiwe mbalimbali lakini mwisho wa siku imetimia ile tarehe iliyopangwa kukutana miamba hiyo, mechi ya leo ni ya marudiano baada ya Oktoba 1 mwaka jana kuumana katika uwanja huo huo wa Taifa na kutoka sare ya kufungana 1-1.

Amissi Tambwe alitangulia kuipatia Yanga bao la kuongoza dakika ya 26 kipindi cha kwanza na Simba wakasawazisha dakika ya 87 kipindi cha pili likifungwa na kiungo Shiza Kichuya kwa kutumbukiza kona iliyokwenda moja kwa moja wavuni.

Kwa maana pambano la leo linatafuta mbabe wa msimu huu, iwe Yanga au Simba mmoja anaweza kuchomoza na ushindi, Lakini Simba wana kumbukumbu nzuri ya kuchomoza na ushindi wa mikwaju ya penalti kule Zanzibar.

Simba iliifunga Yanga kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya kumaliza dakika 90 0-0 mchezo wa nusu fainali kombe la Mapinduzi, Yanga nao wana hasira na kipigo hicho toka kwa Simba lakini pia watatumia mchezo wa leo kumpoza mwenyekiti wao Yusuf Manji ambaye ana misukosuko ya kukamatwa na Polisi akituhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya na kuajiri raia wa kigeni wasio na vibali vya kuishi nchini

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA