Nitabakia Manchester United- Rooney
Nahodha wa Uingereza Wayne Rooney amesema kuwa atasalia katika Klabu ya Manchester United baada ya kuhusishwa na uhamisho wa kwenda China.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 amesema kuwa anatumai kwamba atashirikishwa kikamilifu katika mechi zilizosalia za klabu hiyo msimu huu.
Mkufunzi wa United Jose Mourinho amekataa kukana kwamba Rooney huenda akaondoka klabu hiyo mwezi huu, japokuwa uhamisho huo huenda usikamilike kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho nchini China mnamo tarehe 28 Februali.
"Ni wakati wa furaha kubwa katika klabu hii na ningependa kusalia", alisema Rooney. Wakala wake Paul Stretford alisafiri kuelekea China kuona iwapo atafanikiwa kupata makubaliano japokuwa haijulikani alizungumza na klabu gani.
Mbili kati ya klabu tatu zilizoonekana kuwa klabu mbadala ni Beijing Guoan na Jiangsu Suning zikifutilia mbali uvumi kuhusu uhamisho huo wa Rooney