MANJI ABADILISHIWA SHITAKA, SASA KUFIKISHWA MAHAKAMANI
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
Jeshi la polisi idara ya Uhamiaji limemkuta na hatia Mkurugenzi wa kampuni ya Quality Group na mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Yusuf Manji ya kuwaajili kwenye kampuni yake wafanyakazi wanaoishi nchini na sheria.
Uhamiaji imesema itamfikisha mahakamanj Mkurugenzi huyo na wafanyakazi wake hao ambao waligundulika hivi karibuni wakati jeshi la polisi lilipokwenda kufanya ukaguzi kwenye kampuni hiyo iliyopo pembezoni mwa barabara ya Nyerere.
Ukaguzi huo ulifanyika baada ya Manji kutajwa katika listi ya watu 65 ya washukiwa wa madawa ya kulevya ambapo yeye na Mchungaji Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo waliwahi Alhamisi badala ya Ijumaa siku ambayo walitakiwa kuhojiwa na polisi katika kituo cha kati (Central).
Hata hivyo Manji na Gwajima walishikiliwa kwa siku tatu kabla ya kuachiwa lakini Manji alipelekwa hospitali baada ya kuugua ghafla, Uhamiaji itamfikisha mahakamani mara baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali ambako inadaiwa amelazwa