BARA LA AFRIKA KICHEKO KOMBE LA DUNIA 2026

Rais wa shirikisho la soka duniani (Fifa) Giani Infantino amesema kuwa bara la Afrika litapewa nafasi 7 katika upanuzi wa timu zitakazoshiriki fainali za kombe la dunia mwaka 2016.

Infantino amesema kuwa shirikisho hilo limeongeza uwekezaji wake Afrika kutoka dola milioni 27 hadi 94 kwa mwaka ili kusaidia kukuza mchezo huo, Infantino kwa sasa yuko ziarani nchini Ghana kwa siku moja.

Amekuwa akikutana na rais Akufor Addo na maafisa wakuu wa shirikisho la soka nchini Ghana kuzungumzia hatua za kukuza soka nchini humo, Ziara yake ni mojawapo ya ziara za mataifa kadhaa wanachama wa Fifa

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA