Kiungo Yanga afariki dunia
Na Exipeditor Mataruma. Mbeya
Kiungo wa zamani wa Yanga, Godfrey Bonny "Ndanje" amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Bonny maarufu kama Ndanje amefariki sunia baada ya kulazwa kwa muda mrefu katika Hospitalu ya Makandana, Tukuyu mkoani Mbeya.
Nahodha wa zamani wa Yanga, Shadrack Nsajigwa "Fuso" ambayw alikuwa nahodha wakati Bonny akiichezea Yanga, amethibitisha taarifa hizo pamoja na dada wa marehemu.
"Kweli nimepokea taarifa hizi za masikitiko, ndugu yetu ametangulia mbele za haki, Juhudi zilifanyika lakini Mungu alishapanga yake", alisema.
Kiungo huyo aliichezea Yanga kwa kiwango kikubwa akitokea Tanzania Prisons ya jijini Mbeya. Baada ya kuondoka Yanga alikwenda nchini Nepal ambapo alicheza soka la kulipwa akiwa na Watanzania wengine akiwemo Nsajigwa na Pius Kisambale