Yanga wanasema wao wako vizuri kuliko Simba

Na Ikram Khamees. Kigamboni

Baadhi ya wachezaji wa Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Yanga SC wameiambia Mambo Uwanjani kuwa wao wako vizuri kuliko watani zao Simba SC watakaokutana nao Jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Simba na Yanga zinakutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na zikiwa zimepita siku kadhaa tangu zikutane katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi kule Zanzibar ambapo Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.

Mshambuliaji wa Yanga raia wa Burundi Amissi Tambwe amesema Simba ni timu ya kawaida na haoni ubora wa kuizidi Yanga kwenye mchezo huo, Tambwe amedai Yanga ina kikosi kipana kuliko Simba na kingine kinachowapa jeuri na safu yao ya ushambuliaji.

Nahodha Nadir Haroub "Cannavaro" yeye amekisifu kikosi cha Yanga na kudai kuwa safu ya ulinzi ya Yanga nayo ni imara kwani hadi sasa imeruhusu magoli tisa tu, Cannavaro ameongeza kuwa katika mchezo huo wao ndio watautawala na wana kila sababu ya kushinda.

Mlinzi huyo mwenye bao moja ametambia rekodi nzuri waliyonayo ya kutopoteza mchezo wowote kwenye uwanja wa Taifa tangu msimu uliopita, kufungwa kwa Yanga kwenye uwanja huo no sare na hicho ndicho kinachowapa jeuri, lakini kocha mkuu wa mabingwa hao watetezi Mzambia George Lwandamina yeye ametamba kushinda

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA