Rage awaambia Simba wenzake, waendelee kumuombea Ngoma asipone

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba, Alhaj Ismail Aden Rage ametoa utabiri wake wa pambano la watani wa jadi Simba na Yanga na kusema miamba hiyo itatoka sare katika mchezo huo.

Rage sliyasema hayo leo asubuhi alipozungumza na kituo kimoja cha redio, Rage amedai mechi ya Simba na Yanga itakuwa ngumu na ya ushindani wa aina yake lakini mwisho wa siku miamba hiyo haitaamua mshindi na zitatoka sare iwe ya kufungana au suluhu.

Ameongeza mwenyekiti huyo wa zamani ambaye pia aliwahi kuwa mchezaji wa Klabu hiyo miaka ya 60 na 70, kuwa Simba itaingia katika mchezo huo ikijivunia mabeki wake wa kati ambao hadi sasa wameruhusu magoli saba, wakati Yanga wao wanajivunia safu yao kali ya ushambuliaji.

Rage pia amewataka wapenzi na mashabiki wa Simba kuendelea kumuomba Mungu ili mshambuliaji wa Yanga Mzimbabwe Donald Ngoma asipone haraka, Rage anaamini Ngoma akicheza dhidi ya Simba itakuwa balaa kwani anaijua shughuri yake awapo uwanjani

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA