HUYU HAPA NDIYE ALIYEIKATA UMEME YANGA

Na Prince Hoza. Dar es Salaam

Kama mlidhania Justin Zulu wa Yanga ndiye mkata umeme peke yake basi mnajidanganya, Said Hamisi Ndemla ndiye aliyeikatia umeme Yanga na kupelekea kuchapwa mabao 2-1 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Huo ulikuwa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, katika mchezo huo Yanga ndio walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza lililofungwa na Simon Msuva kwa mkwaju wa penalti baada ya Obrey Chirwa kuangushwa kwenye eneo la hatari, goli hilo lilipatikana dakika ya 6 kipindi cha kwanza.

Yanga walitawala dakika 35 za mwanzo kabla ya Thabani Kamusoko hajaumia na kutolewa nje, benchi la ufundi la Simba SC lilimtoa Juma Luizio na kumwingiza Said Ndemla ambaye aliubadili mchezo na Simba kuuwasha moto na kuelekea mapumziko wakiwa na matumaini kibao.

Kipindi cha pili Simba waliendeleza moto na kuliandama lango la Yanga kama nyuki, kuingia kwa nahodha wao Jonas Mkude kuliendeleza moto na kufanikiwa kusawazisha bao na kuongeza la ushindi, mabao ya Simba yalifungwa na Laudit Mavugo na Shiza Kichuya, kwa hakika Ndemla aliyetakiwa na klabu ya Ligi Kuu ya Sweden ya AFC Eskilistuna ni mkata umeme wa ukweli na masihara

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA