Simba yatinga robo fainali kwa kulipiza kisasi

Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam

Goli lililofungwa na Mrundi Laudit Mavugo limetosha kuipa ushindi Simba SC wa bao 1-0 dhidi ya African Lyon na kutinga hatua ya robo fainali michuano ya Azam Sports Federation Cup au FA Cup katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

African Lyon ikicheza kwa kujilinda zaidi katika kipindi cha kwanza ilijikuta ikifungwa bao hilo lililowaondosha moja kwa moja kwenye michuano hiyo, ushindi wa Simba leo ni kama kulipiza kisasi baada ya kufungwa 1-0 zilipokutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa kwanza mwaka jana.

Simba imetinga hatua ya robo fainali na sasa itaingia kwenye maandalizi ya mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya mahasimu wake Yanga Februali 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Kikosi cha Simba kinachonolewa na Mcameroon Joseph Omog kilionekana kutawala zaidi sehemu ya kiungo na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga isipokuwa washambuliaji wake hawakuwa makini, Laudit Mavugo anaonekana kuimarika kabisa kwani hili ni goli lake la tatu katika mechi tatu alizocheza hivi karibuni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA