Mwamuzi wa Simba na Yanga huyu hapa
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
Hatimaye mwamuzi atakayezihukumu Simba na Yanga kesho Jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam amewekwa hadharani ambaye si mwingine ni Mathew Akrama kutoka mkoani Mwanza.
Akrama anafahamika vema na vilabu hivyo kwani amewahi kuzihukumu misimu kadhaa iliyopita na amekuwa mkali awapo uwanjani, Akrama anakabidhiwa kipyenga wakati miamba hiyo itakapokutana kesho katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Awali jina la mwamuzi lilikuwa kizungumkuti na kuzua sintofahamu na baada ya TFF kuliweka hadharani jina hilo na kutuliza presha ya mashabiki wa vilabu hivyo, Akrama atasaidiwa na Mohamed Mkono na Hassan Zani