Yanga mbioni kuingia mkataba mnono na Tigo

Na Prince Hoza. Dar es Salaam

Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Dar Young Africans SC maarufu Yanga iko mbioni kuingia mkataba mnono wa udhamini na kampuni ya simu za kiganjani ya Tigo imefahamika.

Taarifa ambazo Mambo Uwanjani inazo ni kwamba Tigo wataingia makubaliano na Yanga na huenda kampuni hiyo ikamwaga Shilingi Bilioni 4 kama sehemu ya udhamini huo ambao utaifanya Yanga kuwa Klabu kubwa barani Afrika.

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji aliwaambia Wanayanga kuwa Tigo wataidhamini Yanga hivi karibuni ili angalau Klabu ijiendeshe kimaslahi, Manji pia ndiye mmiliki wa Tigo aliyeinunua kampuni hiyo tangu mwaka 2014 licha ya kuwepo kesi mahakamani ikitaka mauzo yarudiwe tena baada ya kuwepo ubabaishaji.

"Kwa sasa Manji ana matatizo, ngoja yaishe kwanza ndio tutazungumzia", alisema mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji wa Yanga, Manji amelazwa chini ya ulinzi wa polisi wa idara ya Uhamiaji katika hospitali ya Muhimbili Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA