Mkude arejeshwa Simba, kuwavaa Yanga

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Kiungo na nahodha wa Simba hatimaye amerejeshwa tena kikosini baada ya kuwa nje kwa siku kadhaa kufuatia kutofautiana na kocha mkuu wa Simba Mcameroon Joseph Omog.

Mchezaji huyo alikosa mechi mbili za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Majimaji iliyopigwa mjini Songea Simba ikishinda 3-0 na Tanzania Prisons iliyofanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam Simba tena ikishinda 3-0.

Hofu ilianza kutanda kuelekea mpambano wa watani mechi ambayo itachezwa Februali 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, viongozi wa Simba walikutana kuzungumzia mchezo huo lakini wakaona umuhimu wa Mkude kwenye mchezo huo.

Hivyo wakaamua kumrejesha na huenda akawemo kwenye mchezo huo muhimu utakaotoa sura ya ubingwa wa Bara, hata hivyo mchezaji huyo ameridhia kurejea kikosini na kuondoa uvumi kuwa abataka kujiunga na Yanga mwishoni mwa msimu

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA