Mourinho aipa ubingwa Chelsea
Meneja mtukutu wa Manchester United Jose Mourinho amekubali yaishe kwa vinara wa Ligi Kuu ya Primia maarufu EPL, Chelsea kwamba watabeba kikombe msimu huu huku akiiondoa timu yake kwenye mbio hizo.
Mourinho amesema nafasi pekee iliyosalia kwa timu yake ni kushinda kombe la FA ambapo mchezo uliombele yao ni dhidi ya Chelsea, Mreno huyo mwenye rekodi ya aina yake amemsifu meneja wa Chelsea Antoine Conte.
"Chelsea ndio mabingwa wa EPL hilo halina ubishi najipanga kuipa taji la FA, Man U", amesema Mourinho, mpaka sasa Man U inapigania kuingia kwenye Big Four na bado ipo nafasi ya sita