WEMA SEPETU AJIUNGA CHADEMA
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Kada na mwanachama wa Chama Cha Mapjnduzi (CCM) Wema Isaack Abraham Sepetu sambamba na mama yake mzazi kwa pamoja wamejiunga rasmi na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA. leo.
Wema ameamua kukihama CCM chama ambacho alikipigania katika uchaguzi mkuu uluofanyika mwaka 2015, Wema ambaye ni msanii wa filamu na Miss Tanzania wa zamani, ameamua kuachana na CCM kutokana na kukandamizwa kwa demokrasia na uhuru wa kuongea.
Hivi karibuni msanii huyo maarufu alifikishwa mahakamani akituhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya, Wema alitajwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Poul C Makonda, kwa kitendo hicho ambacho kilimfanya mlimbwende huyo kulala mahabusu Central kwa siku nne kumelekea kuachana na CCM ingawa yeye mwenyewe amesema ameamua kukihama kutokana na kukandamizwa kwa demokrasia.
Nao Chadema wamesema wamempokea Wema kwa mikono miwili na wamewataka na watu wengine walioko CCM kumuiga Wema kwani wakati muafaka ni huu, Tayari wasanii kama Joseph Mbilinyi "Mr Two" au Sugu na Joseph Haule "Prof Jay" wamejiunga na chama hicho na sasa ni wabunge wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama hicho