Ranieli atupiwa virago Leicester City

Bingwa mtetezi wa Ligi Kuu England Leicester City imemtimua Kocha wake mkuu, Muitaliano Claudio Ranieli, ikiwa ni miezi tisa baada ya kuiwezesha kupata ubingwa wa Ligi Kuu.

Leicester iko katika nafasi ya 17, na ikipoteza alama moja tu italuwa kwenye mstari wa kushuka daraja, kutimuliwa kwa kocha huyo kumekuja saa 24 baada ya kichapo cha magoli 2-1 walichokipata kutoka kwa Sevilla.

Leicester City msimu uliopita ilitwaa ubingwa kwa zaidi ya alama 10 mbele, lakini msimu huu mpaka sasa wamecheza michezo 25 ya ligi na kushinda mitano pekee, na imesalia michezo 13 ligi kuisha

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA