Kikwete kujenga uwanja wa kisasa Chalinze

Na Shaaban Hussein. Bagamoyo

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete kwa kushirikiana na kampuni ya Ujenzi ya nchini China wamekubaliana kujenga Uwanja wa kisasa maeneo ya Msoga Chalinze mkoani Pwani.

Akizungumza juzi, Kikwete ambaye ni mtoto wa Rais wa Awamu ya nne ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amesema ujenzi huo wa uwanja utatumika kwa ajili ya mchezo wa soka na michezo mingineyo.

Ameongeza kuwa hiyo ni ahadi yake kwa wapiga kura wa jimbo hilo kuwa atawajengea uwanja WanaChalinze, amedai tayari kampuni hiyo imeshaanza harakati za ujenzi na unaweza kukamilika kwa ajili ya mazoezi na hatua nyingine ya uwekaji uzio na majukwaa itafuata.

"Hii ni fulsa kwa wakazi wa Chalinze kwani nimepania kuendeleza michezo kwenye jimbo langu, najua michezo ni ajira hivyo nimeona vema nianze mapema mchakato wa kujenga uwanja, nimeamua kuujenga Msoga ambapo ni nyumbani kwetu lengo ni kuinua michezo", Alisema.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA