Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2017

Vita ya matajiri wawili VPL yamalizwa kwa sare

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dodoma Matajiri wawili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Singida United na Azam FC iliamuliwa kwa sare ya kufungana bao 1-1 jioni ya leo katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. Singida United inayonolewa na Mholanzi Hans Van der Pluijm ilitangulia kupata goli la uongozi lililofungwa na Mrwanda, Danny Usengimana, lakini Azam wakakomboa kupitia Peter Paulo na kufanya timu hizo zigawane pointi moja moja. Kwa matokeo hayo, Azam FC inaendelea kukamata nafasi ya pili ikifikisha pointi 11 ikishika dimbani mara tano, na kushinda mechi tatu, sare mbili, wakati Singida inakamata nafasi ya tatu na pointi zake 10 ikishinda mechi tatu, kufungwa moja na sare moja. Matokeo mengine Ligi Kuu bara kama ifuatavyo. Mwadui FC 2 Mbeya City 2. Mwadui Complex. Shinyanga. Mbao FC 1 TZ Prisons 1, CCM Kirumba. Mwanza. Majimaji 0 Kagera Sugar 0. Majimaji Stadium. Songea. Ruvu Shooting 1 Njombe Mji 1. Mabatini Stadium. Mlandizi. Ndanda 2 Lipuli 1. Nangwanda Sijaona. Mtwara. Yanga 0 M...

YANGA BUTU YALAZIMISHWA SARE NA MTIBWA SUGAR

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Hali si nzuri kwa mabingwa wa soka nchini baada ya kulazimishwa sare tasa na vinara wa ligi hiyo Mtibwa Sugar jioni ya leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Yanga inaonekana wazi kufeli kwenye idara yake ya ushambuliaji kwani imekosa mabao manne ya wazi ambayo yamemfanya kipa wa Mtibwa Sugar, Bennedictor Tinoco kuonekana bora, lawama nyingi zimemuendea Mzimbabwe Donald Ngoma kwa kutokuwa makini na kuifanya Yanga itoke kapa. Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha pointi 9 ikiwa imecheza mechi tano ikifanikiwa kushinda mechi mbili, sare tatu, wakati Mtibwa Sugar wanaendelea kushikilia usukani wa ligi hiyo wakifikisha pointi 11 baada ya mechi tano, nne tatu wakishinda na mbili kwenda sare Donald Ngoma wa Yanga akizuiwa na mchezaji wa Mtibwa, leo, picha kwa hisani ya Bin Zubeiry

KUZIONA TANZANITE, NIGERIA 500 TU

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam TFF  imetoa fursa ya mashabiki wengi kuingia uwanjani kuishangilia Timu ya Taifa ya Wanawake wenye umri wa chini ya miaka 20 ‘Tanzanite’ itakayocheza kesho na Falconets ya Nigeria kwa kuweka kiingilio cha shilingi 500 pekee. Katika mchezo huo utakaofanyika dimba la Azam Complex Chamazi, kiingilio cha shilingi 500 kitakuwa kwa mashabiki watakaoketi eneo la mzunguko huku kwa wale watakaokaa Jukwaa Kuu (VIP) watalipia Shilingi 1,000 pekee Tanzanite watacheza  na Nigeria kesho

Ukweli kuhusu Chirwa kumpiga mwandishi huu hapa

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Ukweli umebainika baada ya mshambuliaji wa Yanga Mzambia, Obrey Chirwa kutaka kumshambulia mwandishi wa gazeti la Mtanzania, John Dande umewekwa hadharani na mmoja wa waandishi ambaye hakutaka kutaja jina lake. Taarifa zimebainika kuwa mwandishi huyo akiwa na kamera yake alimfuata Chirwa ambaye alikuwa anabadilisha nguo ili aanze mazoezi, mwandishi huyo inadaiwa alimpiga picha hiyo ambayo Chirwa hakuridhika na kumfuata kisha kumpa kisago kabla ya Juma Abdul naye wa Yanga kuingilia kati. Hata hivyo mwandishi huyo alizifuta picha hizo baada ya Chirwa kumtaka afanye hivyo, Vyombo vya habari vimepinga vikali kitendo hicho cha Chirwa kumpiga mwandishi huyo. Lakini Mambo Uwanjani ilizungumza na mwandishi huyo ambapo alisema yamekwisha na ameshamsamehe mchezaji huyo ingawa alidai alimpiga picha ya uwabjani na si akibadilisha nguo kama inavyoelezwa Obrey Chirwa akizuiwa na Juma Abdul asimpige mpiga picha John Dande aliyejikinga na begi

YANGA MGUU SAWA KUUA MTIBWA KESHO

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Yanga SC imewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwani kesho watawapa furaha pale watakapoichakaza Mtibwa Sugar katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Mkuu wa kitengo cha Habari na mawasiliano, Dissmas Ten amesema kikosi kipo tayari kuvaana na Mtibwa Sugar na amedai ushindi utapatikana kwani maandalizi yamekamilika. Yanga ikiwategemea zaidi washambuliaji wake Donald Ngoma, Obrey Chirwa, Ibrahim Ajibu, Emmanuel Martin na Thabani Kamusoko itataka kuwathibitishia mashabiki wake kuwa wataibuka na ushindi ili angalau kusogea mbele kwenye msimamo wa ligi. Yanga itamkosa kiungo wake mkabaji, Mkongoman Papy Kabamba Tshishimbi ambaye ana kadi tatu za njano, Rekodi zinaonyesha Yanga imekuwa ikipata matokeo mazuri inapokutana na Mtibwa katika uwanja wa Taifa ama Uhuru jijini Dar es Salaam Yanga SC wapo tayari kuilaza Mtibwa kesho

ANCELOTTI AFURUSHWA BAYERN MUNICH

Picha
Kocha wa mabingwa watetezi wa Bundesliga Bayern Munich, Carlo Ancelotti ametimuliwa, ikiwa ni siku moja baada ya kufungwa mabao 3-0 na PSG kwenye ligi ya mabingwa Ulaya, “ Champions League”. Ancelloti alijiunga na Bayern msimu uliopita na kuchukua ubingwa wa Bundesliga, lakini aliondolewa katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa ya 2016/17 na Real Madrid. Inasemekana kutimuliwa kwake kumetokana na kuondoshwa huko katika michuano hiyo mikubwa Ulaya kwani kiu kubwa kwa mashabiki wa Bayern ilikuwa ubingwa wa Ulaya na matumaini ya timu hiyo yameyeyuka Carlo Ancelotti amefutwa kazi

RATIBA YA LIGI KUU BARA MWISHONI MWA WIKI HII HAPA

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaendelea tena mwishoni mwa juma hili ambapo karibu timu zote zitashuka viwanjani kukamilisha mzunguko wa tano wa ligi hiyo inayoshika kasi. Tayari timu tatu zinachuana juu kileleni huku kwa mara ya kwanza miamba Simba na Yanga zikiondoshwa katika kinyang' aanyiro hicho, mchuano huo unahusisha Mtibwa Sugar ambao ni vinara, Azam FC na Singida United Ratiba hiyo inaonyesha Jumamosi kutachezwa mechi saba na Jumapili itachezwa mechi moja, ebu itazame ratiba kamili. Jumamosi Septemba 30 Majimaji FC vs Kagera Sugar, (Majimaji Stadium, Songea) Singida United vs Azam FC, (Jamhuri Stadium, Dodoma) Ndanda FC vs Lipuli FC, (Nangwanda Stadium, Mtwara) Yanga SC vs Mtibwa Sugar, (Uhuru Stadium, Dar es Salaam) Mwadui FC vs Mbeya City, (Mwadui Complex, Shinyanga) Mbao FC vs TZ Prisons, (CCM Kirumba, Mwanza) Ruvu Shooting vs Njombe Mji FC, (Mabatini Stadium, Mlandizi) Jumapili Oktoba 1 Stand United vs Simba SC, (CCM Kam...

STAA WETU:

Picha
AZISHI SIMON PETRO: KIPA ALIYEMKIMBIA JUMA KASEJA MBEYA CITY, AFUNGUKA MAKUBWA. Na Prince Hoza UNAJUA unaweza usiamini lakini ndiyo ulivyo ukweli, kuwa mlinda mlango Azishi Simon Petro aliikacha Mbeya City mara baada ya kusajiliwa kipa mkongwe aliyepata kuzichezea Simba na Yanga, Juma Kaseja. Unajua ilikuwa hivi, Azishi alisajiliwa na Mbeya City kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Kimondo FC nayo ya Mbeya, Azishi ambaye alifanya mahojiano na mwandishi wa makala hii kuwa alilazimika kuondoka Mbeya City kwakuwa hakulipwa mishahara ya miezi mitatu na pesa yake ya ada ya usajili. Anasema Mbeya City walikuwa wanamzungusha kumlipa fedha zake za usajili ambazo ni shilingi Milioni 5, huku pia wakimpiga danadana kumlipa mshahara wake, lakini akashangaa kuona uongozi wa Mbeya City ukimleta Juma Kaseja ambaye alikuwa amevunjiwa mkataba wake na Yanga, kitendo hicho kilimuuma sana na akaamua kurejea Kimondo FC iliyokuwa Daraja la kwanza. Huyo ndiye Azishi Simon Petro aliyezaliwa Mdaula, ...

ALIYETAKA KUMTOA ROHO EMMANUEL MARTIN WA YANGA ASIMAMISHWA LIGI KUU

Picha
Na Shafih Matuwa. Dar es Salaam Kamati ya masaa 72 ya Bodi ya uendeshaji wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, leo imetoa hukumu mbalimbali na kufikia maamuzi ambapo imemsimamisha mchezaji wa Majimaji ya Songea, Juma Salamba kwa kitendo chake cha kumpiga kiwiko kiungo mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Martin katika mchezo wa ligi uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 uwanja wa Majimaji mjini Songea. Martin ambaye aliingia kuchukua nafasi, alijikuta akipigwa kiwiko na kusababisha apoteze ufahamu wake wa akili (Kuzirai) ambapo alikimbizwa hospitali, Martin alikuwa msaada kwa Yanga katika mchezo huo ambapo kuingia kwake kulipelekea Yanga kusawazisha goli. Salamba amesimamishwa na kamati hiyo huku kesi yake ikisikilizwa, Hata hivyo Martin amerejea tena uwanjani na anaendelea kuichezea timu yake, wakati Salamba akisimamishwa, mwamuzi wa mchezo huo naye amepewa adhabu kwa sababu alishindwa kumuonya mchezaji aliyemdhuru mwenzake uwanjani Juma Salamba wa Majimaji amesimamishwa

TID kugombea Ubunge mwaka 2020

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Mwanamuziki maarufu wa Bongofleva, Khalid Mohamed "TID" amesema atawania ubunge ifikapo mwaka 2020 endapo atapata ridhaa kutoka kwa wazee. TID ameyasema hayo asubuhi ya leo akihojiwa na Efm ambapo amedai atagombea nafasi hiyo endapo wazee watampa baraka zote, TID amedai atagombea ubunge katika jimbo la Kinondoni ambapo ndipo anapoishi. Msanii huyo aliyepata kutamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo "Zeze", "Siamini" na nyinginezo, amewahi kutuhumiwa madawa ya kulevya na alikamatwa katikati ya mwaka huu na kufunguliwa mashitaka na serikali kuhusu matumizi ya dawa hizo yeye na wasanii wenzake TID atagombea Ubunge mwaka 2020

SIMBA WAAPA KUIMALIZA STAND UNITED KWAO

Picha
Na Paskal Beatus. Mwanza Mabingwa wa Ngao ya Jamii, Simba SC wamesema safari hii hawatafanya makosa katika mchezo wao wa ligi dhidi ya Stand United utakaopigwa katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga. Simba wanajifua jijini Mwanza ambapo wameweka kambi yao kwa ajili ya mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wake, Simba ilitoka kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Mbao FC mchezo uliofanyika uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza. Pia Simba ikaenda Tabora kucheza mechi ya kirafiki na Milambo na kulazimishwa sare ya 0-0, na mashabiki wa Simba wakaanza kumshutumu kocha Mcameroon, Joseph Omog ambapo wamekuwa wakitaka aondolewe, lakini uongozi wa Simba unamkingia kifua na mara kwa mara msemaji wa timu hiyo Haji Manara amekuwa akisema kocha huyo aondoki. Kuelekea mchezo huo dhidi ya Stand United Jumamosi ijayo, msemaji wa timu hiyo Haji Manara amesema Stand United lazima ife nyumbani kwao kwakuwa wamejipanga kushinda mchezo huo na hakuna kitakachowafanya wasipate ushindi Wacheza...

Mtibwa Sugar waanza kuchonga

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Mtibwa Sugar kupitia kwa msemaji wao Tobias Kifaru amesema kikosi chake kitaondoka na pointi tatu dhidi ya Yanga na kuendelea kuongoza ligi. Kifaru amesema amekiona kikosi cha Yanga kinavyocheza anadhani timu yake itapata ushindi mkubwa kwani Yanga si lolote si chochote na kwa uchezaji wao sidhani kama watapata hata sare siku hiyo. Hata hivyo rekodi inaibeba zaidi Yanga kwani timu hizo kila zinapokutana hasa katika Uwanja wa Taifa ama Uhuru jijini Dar es Salaam ni Yanga pekee imekuwa ikipata matokeo mazuri hivyo inaipa ugumu Mtibwa kuelekea katika mchezo huo Mtibwa Sugar wameanza tambo dhidi ya Yanga

Singida United yaipigia hesabu kali Azam FC

Picha
Na Paskal Beatus. Dodoma Kocha mkuu wa Singida United, Hans Van der Pluijm raia wa Uholanzi amesema kwa sasa hesabu zao wanazielekeza kwa Azam FC ambao watapambana nao mwishoni mwa wiki katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Pluijm ambaye ni kocha wa zamani wa Yanga SC, amedai kikosi chake kinahakikisha kinapata ushindi kila mechi hivyo anaumiza kichwa kwa Azam kwakuwa timu hiyo hadi sasa haijaruhusu hata bao lakini amewapa maelekezo ya kutosha wachezaji wake ili waweze kufunga watakapokutana. Mpaka sasa Singida United inakamata nafasi ya tatu ikiwa na pointi tisa lakini Azam FC wao wanakamata nafasi ya pili wakiwa na pointi kumi na hawajaruhusu nyavu zao kutikiswa lakini wamefunga magoli matatu tu. Kocha wa Singida United anajivunia safu yake ya ushambuliaji kwani hadi sasa imeshafunga mabao matano ambayo yanawapa jeuri ya kushinda mbele ya Azam FC Jumamosi ijayo Singida United wakipasha

ZFA YAISHIKA PABAYA TFF KUHUSU UTEUZI WA TIMU YA TAIFA

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Chama cha soka visiwani Zanzibar (ZFA) kimelishutumu Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, (TFF) kwa kutoshirikisha wachezaji wa Zanzibar kwenye uteuzi wa timu ya taifa, Taifa Stars na kumshangaa kocha mkuu wa timu hiyo Salum Mayanga akiita wachezaji 22 bila kuwemo wachezaji kutoka visiwani humo. Zanzibar imeondolewa uanachama wake na Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika, (CAF) kwa vile ni sehemu ya Tanzania hivyo haitaweza kushiriki michuano ya mataifa Afrika yanayoshirikisha timu za taifa. Kwa maana hiyo wanatakiwa kuunda timu moja ya taifa kupitia jamhuri ya muungano, lakini Zanzibar wanatengwa na TFF na wameamua sasa kuishutumu hadharani TFF na wanataka kukutana na Rais wa Shirikisho hilo ili kuzungumzia kero hiyo. Akizungumza leo, makamu wa Rais wa ZFA, Ally Mohamed amesema umefika wakati sasa kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars atembelee visiwani na kuteua wachezaji kupitia ligi yao na si kukimbilia wavhezaji wanaocheza Simba,Yang...

Kipa bora wa Airtel Rising Star apata shavu Qatar

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Kipa bora wa mashindano ya vijana ya Airtel Rising Star, Alfan Romanus amepata nafasi ya kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini Qatar ambapo tayari timu ya Spays Academy tayari inamuhitaji. Akizungumza na Mambo Uwanjani, Romanus ambaye aliibuka kuwa kipa bora wa mashindano hayo, anatazamiwa kuondoka Oktoba 20 mwaka huu tayari kabisa kuanza majaribio yake. Endapo Romanus atafuzu majaribio hayo atakuwa ameungana na Mbwana Samatta, Farid Mussa, Thomas Ulimwengu, Elius Maguli, Simon Msuva na Abdi Banda ambao wanacheza soka la kulipwa ughaibuni Alfan Romanus, kipa bora wa Airtel Rising Star ameula Qatar

Kichuya naye arejea mdogo mdogo kikosini

Picha
Na Mwandishi Wetu Kiungo mshambuliaji wa mabingwa wa Ngao ya Jamii, Simba SC, Shiza Ramadhan Kichuya leo ameungana na wenzake katika mazoezi ya timu hiyo inayojiandaa na mchezo wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Kichuya ameanza mazoezi lakini akiwa chini ya daktari wa klabu hiyo, mchezaji huyo aliumia katika mchezo wa ligi dhidi ya Mbao FC uliofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Simba ikilazimishwa sare ya mabao 2-2 huku Kichuya akiwa mfungaji wa goli la kwanza la Simba. Mchezaji huyo alitolewa nje baada ya kuumizwa na wachezaji wa Mbao, huenda akawemo katika kikosi kitakachoanza dhidi ya Stand United utakaofanyika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga, Simba ina pointi nane na inahitaji ushindi ili kusonga mbele kwenye ligi hiyo Shiza Kichuya ameanza mazoezi leo baada ya kuumia

LWANDAMINA ACHEKELEA KUREJEA KWA TAMBWE KIKOSINI

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Kocha mkuu wa mabingwa wa soka nchini, Yanga SC, Mzambia George Lwandamina, amefurahia kurejea kwa straika Amissi Tambwe raia wa Burundi katika kikosi chake. Tambwe alikosekana kwa muda mrefu baada ya kuumia mazoezini visiwani Pemba wakati Yanga ilipoenda kuweka kambi kujiandaa na mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wao Simba. Lwandamina amefurahia urejeo wa Tambwe kwakuwa ni mahiri kwa kufunga hivyo kikosi chake kitakuwa kikipata matokeo mazuri, Yanga imekuwa ikishinda ushindi mwembamba hivyo Tambwe anaweza kuwapa raha mashabiki wa Yanga. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Vital'0 ya Burundi na Simba ya Tanzania, amewahi kuwa mfungaji bora wa VPL mara mbili akiwa Simba alichukua ufungaji bora kwa kufunga magoli 19 na Yanga aliweza kufunga magoli 21, Tambwe ameanza mazoezi mepesi na huenda akawemo katika kikosi cha Yanga kitakachocheza na Mtibwa Sugar Jumamosi ijayo Amissi Tambwe amerejea kikosini Yanga

Samatta amshukuru Mwaisabula

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji katika klabu ya KRG Genk, Mbwana Ally Samatta amesema hatomsahau kamwe kocha wake wa zamani Kenny Mwaisabula "Mzazi" kwani ndiye aliyemsaidia kumpa ujasili mpaka leo hii amefikia kuwa staa mkubwa wa kuaminiwa na klabu kubwa kama Genk. Samatta aliandika maneno hayo kupitia ukurasa wake wa facebook ambapo amemmwagia sifa kemkem Mwaisabula ambaye pia amewahi kuzifundisha Bandari Mtwara, Cargo na Yanga SC. "Kennedy mwaisabula "mzazi" heshima yako sana najua unajua kuwa nakuheshimu ila inawezekana ujui ni kwa kiasi gani,umenijengea moyo mgumu na wenye kutokukata tamaa kila siku ktk soka kwa lile ulilolifanya wakati ule nikiwa bado mdogo kbsa. "Siku ambayo sikulala usingizi nikihofia mechi baada ya "mzazi" kuniambia kuwa mechi ya kesho utaanza. Nadhan unaikumbuka taifa cup basi siku iyo ilikuwa "temeke na mbeya" wkt bado nip...

Mbeya City wapata kocha mpya

Picha
Na Exipeditor Mataruma. Mbeya Wagonga nyundo wa Mbeya City wa jijini Mbeya hatimaye wamemtangaza kocha wao mpya baada ya kuachana na Mmalawi, Kinnah Phiri hivi karibuni. Taarifa iliyotolewa jana usiku na uongozi wa timu hiyo umesema umemsainisha mkataba wa mwaka mmoja aliyewahi kuwa mshauri wa ufundi katika timu ya taifa ya Burundi Nsanzurwino Ramadhan kuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Ramadhan amewahi pia kufundisha soka katika nchi za Rwanda, Kenya, Afrika Kusini na Burundi pia. Mrundi huyo sasa anakuwa kocha wa tatu kuinoa timu hiyo baada ya Juma Mwambusi na Kinah Phiri, Mohamed Kijuso ambaye zamani amewahi kuichezea Simba SC ataendelea kuwa kocha msaidizi Nsanzurwino Ramadhan, kocha mpya wa Mbeya City

Serikali yafuta Miss Tanzania na tuzo za Kill

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Serikali imefuta rasmi mashindano ya Miss Tanzania na yale ya kuwania tuzo za muziki za Kilimanjaro Music Award kwa madai zimekuwa zikiendeshwa kwa ubabaishaji mkubwa huku wanaoshinda inadaiwa wamekuwa wakipendelewa. Hivyo sasa imeamua kuingilia kati na kusitisha mashindano yake na itapanga utaratibu mpya kabla hayajaanza upya, hayo yameamuliwa na wizara ya Habari, Michezo, Utamaduni na Sanaa kupitia kwa waziri wake Dk Harrison Mwakyembe. Serikali imefikia maamuzi hayo baada ya kusikiliza malalamiko ya wadau juu ya uendeshaji wa mashindano hayo pamoja na kugubikwa na ubabaishaji katika utoaji wa zawadi kwa washindi, serikali imewataka waandaaji kuwasilisha zawadi kwao mapema kabla mashindano hayajaanza Waziri Mwakyembe amesitisha Miss Tanzania

Mourinho kutoadhibiwa tena na FA

Picha
Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho hatochukuliwa hatua zaidi baada ya kutimuliwa uwanjani na mwamuzi Claig Pawson Jumamosi wakati timu yake ilipocheza EPL. Taarifa zaidi kutoka kwa Shirikisho la mpira wa miguu FA limesema adhabu ya kukosa mechi mbili kwa mkufunzi huyo inatosha na hawatamuadhibu tena. Wengi walitegemea Mourinho angepata adhabu kubwa zaidi ya kufungiwa lakini FA imesema hatoadhibiwa tena kwani kifungo cha kukosa mechi mbili ni kikubwa kwake Jose Mourinho hatoadhibiwa tena

MANJI AFUNGUKA MAZITO MAHAKAMANI, AKIRI KUTUMIA MADAWA

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Mehbood Manji amefunguka mambo makubwa mahakamani wakati wa kusikilizwa kwa shauri lake la kutumia madawa ya kulevya. Manji ambaye alikamatwa na jeshi la polisi na kushikiliwa kwa muda amekiri ni kweli anatumia madawa ya aina ya Morphiem na Benzodiazepines ambazo zinamsaidia kwa matatizo ya moyo. Manji amefunguka hayo katika mahakama ya Kisutu  leo kuwa amekuwa akitumia dawa hizo kwa muda mrefu na zimekuwa zikimtibu maradhi ya moyo ambayo yamekuwa yakiitesa familia yao kwa miaka mingi na yeye aligundulika kuwa na ugonjwa huo tangu akiwa na miaka 26. Aidha mwenyekiti huyo wa zamani wa Yanga amelilalamikia jeshi la polisi kwa kitendo chake cha kwenda kukagua nyumbani kwake na kuchukua kompyuta yake iliyokuwa na nyaraka za bisshara xake, Manji pia amesema mbali na kuchukuliwa kompyuta yake pia simu na vitu vyake vingine navyo vilibebwa na polisi hao na hadi sasa bado hajarudishiwa Yusuf Manji

Makala ya Kispoti

Picha
TUNAPANDAJE VIWANGO KWA KUCHEZA NA MALAWI! Na Prince Hoza KWANINI Watanzania hasa wapenda soka wanaendelea kumkumbuka Rais Leodegar Chila Tenga ni kwa sababu aliiwezesha timu ya taifa, Taifa Stars kucheza na vigogo wa soka barani Afrika, wakumkumbuka mwingine ni aliyekuwa kocha wa timu hiyo Mbrazil Marcio Maximo. Kingine labda niseme kocha wa sasa wa Taifa Stars, Salum Shaaban Mayanga ni muoga wa mechi, labda hapo naweza kueleweka kidogo maana tumechoka kusikia timu yetu ya taifa kila inapokuja kalenda ya FIFA tunacheza na Malawi au Burundi. Nasema tumechoka, mwezi ujao wa Oktoba 7 mwaka huu, Taifa Stars itacheza na Malawi mchezo wa kirafiki unaotambuliwa na FIFA, mchezo huo utafanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Kwa maana hiyo Stara inaingia kambini Oktoba 1 Jumapili ijayo na Oktoba 7 watacheza na The Flame, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itasimama kupisha mchezo huo, tayari kocha Mayanga ameita wachezaji 22 kwa ajili ya mchezo huo. Mayanga ameshindwa kuwasha...

Simba yalazimishwa sare na kitimu kisichojulikana

Picha
Na Mwandishi Wetu. Tabora Simba SC jioni ya leo imeshindwa kutamba mbele ya kitimu cha daraja la pili, Milambo FC baada ya kutoka suluhu 0-0 mchezo wa kirafiki katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora. Mabingwa hao wa Ngao ya Hisani walishindwa kabisa kutawala eneo la kiungo licha ya kushusha kikosi chake chote ambacho kikajikuta kinakamatwa na wasiojulikana hao wa Milambo ambao wanatafuta nafasi ya kurejea Ligi Kuu Bara tangu enzi za Rais Benjamin Mkapa walipokuwa wanashiriki ligi hiyo, Simba wapo Tabora kwa maandalizi ya mchezo wao wa ligi dhidi ya Stand United. Simba leo ilimchezesha kwa mara ya kwanza kiungo wake Jonas Mkude ambaye alianza mwanzo hadi mwisho akisaidiana na Mnyarwanda Haruna Niyonzima ambaye alishindwa kufurukuta mbele ya vijana hao wasiojulikana wa Milambo Milambo FC imeibana Simba leo

Mtibwa Sugar yashikwa na Ruvu Shooting lakini bado vinara Ligi Kuu Bara

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Licha ya Azam FC kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Lipuli FC bao likifungwa na Mbaraka Yusuph usiku huu katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi, lakini Mtibwa Sugar wameendelea kubaki kileleni ingawa jioni ya leo imebanwa na maafande wa Ruvu Shooting ya Mlandizi Pwani baada ya kufungana bao 1-1. Mtibwa Sugar  ililazimika kusawazisha baada ya Zubeir Dabi wa Ruvu kutangulia kufunga kabla ya Stamili Mbonde kukomboa. Mechi nyingine zilipigwa ambapo Stand United ilipata ushindi wake wa kwanza dhidi ya Mbeya City 2-1 uwanja wa Kambarage wakati Singida United imeifunga Kagera Sugar 1-0. Bao pekee la Singida United lilifungwa kwa mkwaju wa penalti na Mzimbabwe Tafadzwe Kutinyu na sasa Singida United chini ya Mholanzi Hans Van Pluijm sasa imefikisha pointi tisa ikiwa katika nafasi ya tatu nyuma ya vinara Mtibwa wenye pointi 10, Azam FC nafasi ya pili nao wana pointi 10 huku Prisons ikikamata nafasi ya nne na Simba na Yanga zinafuata Mtibwa Sugar leo...

CAF YAIPOKA KENYA UENYEJI WA CHAN

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Shirikisho la kabumbu Barani Africa  CAF limeinyang'anya uenyej wa Fainali za Mataifa barani Afrika kwa wachezaji wa Ndani (CHAN) Kenya ambapo ilipangwa kufanyika nchini humo mwakani 2018. CAF imeingiwa na hofu Kutokana Na Miundo Mbinu ya Nchi hiyo kutoridhisha  na Pia Ukarabati wa Viwanja Haujakamilika hadi Sasa. Hilo ni funzo kwa nchi zinazopewa nafasi ya kuandaa fainali za michuano mbalimbali ya CAF kuwa makini kukamilisha miundo mbinu yake ili yasije kutokea kama kwa Kenya ambao walipewa nafasi hiyo CAF wameipoka nafasi Kenya

Kiungo Yanga, aachia video ya "Wanatupa watoto"

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Kiungo wa zamani wa Yanga B, Abdul Zen "Okocha" amekamilisha video ya wimbo wake wa miondoko ya Hip hop "Wanatupa watoto" ambayo tayari ameisambaza katika mitandao ya kijamii na imepokelewa vema na mashabiki wake. Abdul  Zeni amewahi kuichezea Yanga B wakati ule ikinolewa na marehemu Tambwe Leya na ilikuwa kidogo apandishwe kwenye kikosi cha wakubwa isipokuwa aliumia, na sasa amegeukia muziki wa kizazi kipya na tayari ana albamu. Tayari msanii huyo ameshatambulisha video yake nyingine ya wimbo wa mapenzi lakini video ya wimbo huu unaohusu utupaji wa watoto, Abdul Zeni ameonyesha masikitiko yake kwa watu wenye tabia ya kutupa watoto hasa vichanga Abdul Zeni, mchezaji wa zamani wa Yanga ambaye kwa sasa anajisghurisha na muziki

Mji Njombe yafufuka Songea

Picha
Na Paskal Beatus. Songea Baada ya kuondokewa na kocha wake mkuu Hassan Banyai, leo timu ya Njombe Mji FC ya mkoani Njombe imepata ushindi wake wa kwanza baada ya kuilaza Majimaji bao 1-0 katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea. Bao pekee la Njombe Mji limefungwa na Jimmr Shoji, matokeo mengine ya ligi hiyo ni kama ifuatavyo, Mwadui FC 1, Tanzania Prisons 3 (Mwadui Stadium, Yanga 1 Ndanda FC 0, kesho Jumapili ligi hiyo itaendelea tena kwa mechi nne kupigwa. Azam FC wataialika Lipuli katika uwanja wao wa Azam Complex pale Chamazi, wakati Ruvu Shooting watawakaribisha Mtibwa Sugar, Stand United watawaalika Mbeya City pale Kambarage Syadium na Singida United watachuana na Kagera Sugar uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Kikosi cha Mji Njombe ambacho jioni ya leo kimefufuka kwa kuilaza Majimaji ya Songea (Picha na Paskal Beatus)

YANGA YAPATA USHINDI MWEMBAMBA, NGOMA AUMIA TRNA

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Yanga SC leo imepata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda FC "Wanakuchele" katika mchezo mkali wa kusisimua uliopigwa jioni ya leo Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Kwa ushindi huo Yanga imefikisha pointi nane ikiwa sawa na mahasimu wao Simba, goli pekee la ushindi la mabingwa hao watetezi lilifungwa na Ibrahim Ajibu akiunganisha krosi ya beki Kevin Yondan ambaye alitumia vema mpira wa kona alioanzishiwa na Juma Abdul, hata hivyo mshambuliaji Mzimbabwe Donald Ngoma aliumia na kutolewa nje ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Emmanuel Martin. Ndanda leo wamecheza vizuri na kuipania Yanga ambapo kama si mabeki wa Yanga kuwa wajanja na kudhibiti mashambulizi ya Ndanda huenda mchezo huo ungeamuliwa na sare, Ndanda walikosa mabao ya wazi, kiungo wa Yanga, Mkongoman Papy Kabamba Tshishimbi alionyeshwa kadi ya njano ya tatu mfululizo na atakosekana katika mchezo ujao dhidi ya Mtibwa Sugar Wachezaji wa Yanga wakimpongeza Ibrahim Aji...

Ajibu, Manyika warejeshwa tena Stars

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Kocha mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars, Salum Shaaban Mayanga amemresha tena mshambuliaji Ibrahin Ajibu wa Yanga na kipa Peter Manyika wa Singida United katika kikosi chake kitakachojiandaa na mchezo wa kirafiki unaotambuliwa na FIFA, dhidi ya Malawi Oktoba 7 mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Katika kikosi hicho, Mayanga ameita wachezaji watano wa kimataifa ambao wanacheza soka la kulipwa nje ya Tanzania , kikosi cha Stars kinaundwa na makipa, Aishi Manula {Simba SC), Ramadhan Kabwili (Yanga SC) na Peter Manyika (Singida United). Mabeki ni Gardiel Michael (Yanga SC), Boniphace Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Kevin Yondan (Yanga SC), Salim Mbonde (Simba SC), Erasto Nyoni (Simba SC), Adeyun Ahmed (Kagera Sugar). Viungo ni Himid Mao ambaye ni nahodha msaidizi, (Azam FC), Hamisi Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Muzamil Yassin (Simba SC), Raphael Daudi (Yanga SC), Simon Msuva (Difaa El Jadida/Morocco), Shiza Kichuya (Sim...

YANGA NA NDANDA NI KUFA NA KUPONA

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaendelea tena leo kwa mechi nne kupigwa katika miji tofauti, lakini mpambano unaovuta hisia za wengi ni kati ya mabingwa watetezi Yanga na Ndanda FC "Wanakuchele" wamakonde wa kutoka Mtwara. Mchezo huo utapigwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jiji la Wazaramo kuanzia saa kumi jioni huku timu zote zikihaha kusaka ushindi, Yanga ambao ni mabingwa watetezi wanataka kushinda ili kuikamata Simba yenye pointi nane. Yanga inataka kushinda mchezo huo ili kuwafurahisha mashabiki wake hasa baada ya kulazimishwa sare na Majimaji ya kufungana bao 1-1 katika uwanja wa Majimaji mjini Songea sare ambayo ilizua minong' ono ya hapa na pale Yanga wanacheza na Ndanda jioni ya leo

YANGA BILA TAMBWE TENA KUWAVAA NDANDA KESHO

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Yanga SC itaendelea kumkosa mshambuliaji wake hatari Amissi Joselyin Tambwe raia wa Burundi katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhdi ya Ndanda FC Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Tambwe amekosa mechi tatu sasa na kesho pia ataendelea kukaa nje akiuguza majeraha ya goti na daktari wa Yanga, Edward Bavu anathibitisha kuwa Yanga ina majeruhi mmoja tu ambaye ni Tambwe, lakini Dissmas Ten ambaye ni msemaji wa klabu hiyo amedai ushindi ni lazima. Yanga inahitaji ushindi ili kufikisha pointi nane na kuisogelea zaidi Simba ambayo jana ilishikwa shati na Mbao FC kwa kufungana mabao 2-2 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Ten amedai washambuliaji wa Yanga wakiongozwa na Donald Ngoma, Obrey Chirwa, Thabani Kamusoko na Ibrahim Ajibu wana kila sababu ya kuhakikisha Yanga inapata matokeo mazuri na kujiimarisha katika msimamo wa ligi

Ndanda waapa kuizuia Yanga kesho

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Wachezaji wa timu ya soka ya Ndanda FC "Wanakuchele" ya mjini Mtwara wameapa kuisimamisha Yanga SC katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaofanyika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam kesho Jumamosi. Ndanda imekuwa ikiizuia Yanga mara kwa mara zinapokutana hivyo watafanya kweli hiyo kesho, Yanga ilitoka kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Majimaji mchezo uliofanyika mjini Songea na kuwafanya wafikishe pointi 5. Kikosi hicho cha Wanakuchele, wameiambia Mambo Uwanjani kuwa mchezo wa kesho wameuchukulia umuhimu wa hali ya juu wakiamini watapata ushindi ili kuwapa matumaini mashabiki wao Wachezaji wa Ndanda wakipasha kwa mara ya mwisho kabla ya kuwavaa Yanga, kesho

STAA WETU:

Picha
ABBAS PIRA: MTANZANIA ANAYECHEZA SOKA ENGLAND, MAYANGA AMTUPIA MACHO. Na Prince Hoza. INAWEZEKANA mafanikio ya Mtanzania Mbwana Ally Samatta yamekuwa kichocheo cha Watanzania wengine wanaocheza nje ya nchi kurejea nyumbani huku wakiwa na shauku kubwa ya kutaka kukipiga kwenye timu yao ya taifa. Tatizo hapa ni profile zao kutokuwa wazi hususani wale waliondoka Tanzania wakiwa vijana wadogo, Abbas Pira ni Mtanzania mzaliwa wa barabara ya tatu jijini Tanga, Mtoto wa tajiri anayemiliki visima vya mafuta jijini humo, Gulam Pira. Abbas Pira ni mchezaji wa zamani wa Coastal Union msimu wa 2002/03 na 2004 akiwa chini ya aliyekuwa kocha mkuu wakati huo marehemu Zakaria Kinanda "Sacchi". Pira aliondoka Tanzania msimu wa mwaka 2006 akiwa na umri wa miaka 17 na kwenda nchini Uingereza kwa ajili ya masomo ya juu, Akiwa London, Uingereza Abbas Pira, aliendelea kucheza soka kwenye mitaa mbalimbali ya jiji hilo. Akiwa huko alicheza vilabu kama Hillington FC, FC Wibledon pamoja n...

Ligi Kuu Bara kuendelea tena mwishoni mwa wiki

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Baada ya leo kuchezwa mchezo mmoja wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam na Mbao FC ya Mwanza uliopigwa katika uwanja wa CCM Kirumba na timu hizo kutoka sare ya kufungana mabao 2-2. Ligi hiyo itaendelea tena Jumamosi na Jumapili kwa timu zote kukutana na kukamilisha mzunguko wa nne. Jumamosi ni, Yanga Vs Ndanda FC, Uhuru Stadium, Singida Vs Kagera Sugar. Jamhuri mjini Dodoma, Mwadui FC Vs Prisons. Mwadui Shinyanga na Majimaji Vs Njombe Mji. Majimaji Songea. Jumapili, Ruvu Shooting Vs Mtibwa Sugar, Mabatini, Mlandizi, Stand United Vs Mbeya City. Kambarage, Shinyanga na  Azam Fc Vs Lipuli Fc. Azam Complex  Dar es Salaam Moja ya mechi za ligi ambayp inaendelea mwishoni mwa juma hili

SIMBA YANG' ANG' ANIWA NA MBAO, CCM KIRUMBA

Picha
Na Paskal Beatus. Mwanza Mabingwa wa Ngao ya Jamii, Simba SC jioni ya leo wameshikwa shati na Mbao FC baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba. Simba ilitangulia kwa bao la winga Shiza Ramadhan Kichuya ambalo lilidumu hadi mapumziko, kipindi cha pili Mbao wakasawazisha kupitia  mshambuliaji wake chipukizi Habibu Kiyombo kabla Simba hawasawazisha kupitia kiungo wake Mghana, James Kotei. Mbao wakasawazisha kupitia kwa Emmanuel Mvuyekire kwa shati la mbali na kufanya matokeo yawe sare ambayo inawafanya Simba kubaki katika nafasi yao ya pili nyuma ya Mtibwa Sugar wenye pointi 9 huku Simba ikiwa na pointi 8. Kwa matokeo hayo Simba itakuwa hatarini kupokwa nafasi hiyo na Azam FC au Singida United endapo zitashinda mechi zao za mwishoni mwa wiki, leo Emmanuel Okwi alipotezwa kabisa na vijana Wavhezaji wa Simba wakiwa hoi

VICENT KIGOSI "RAY" AULA KAMATI YA MASOKO YANGA

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Kaimu mwenyekiti wa mabingwa wa soka nchini, Yanga SC, Clement Sanga ametangaza kuunda kamati saba zitakazoshughurika na masuala ya maendeleo katika klabu hiyo huku msanii maarufu wa filamu hapa nchini. Vincent Kigosi maarufu Ray akitajwa kwenye kamati ya masoko kama mjumbe. Sanga ametangaza kuunda kamati saba jioni ya leo alipozungumza na waandishi wa habari huku majina ya wachezaji wa zamani wa klabu hiyo nao wakitajwa, pia mbali na msanii Ray kutajwa. Msanii mwingine Haji Mboto naye ametajwa kwenye kamati hiyo, Ray na Mboto ni wakereketwa wakubwa wa Yanga hivyo kuwemo kwao kwenye kamati hiyo kutasaidia kukua kwa soko la Yanga katika masuala ya kuvutia wawekezaji. Wachezaji wa zamani ambao wamejumuhishwa kwenye kamati zilizotajwa ambazo ni za kushughurika na masuala ya uwanja wa Kaunda, jengo la mtaa wa Mafia, masoko, Ufundi na nyinginezo ni Aoron Nyanda, Charles Boniface Mkwasa, Kenneth Mkapa, Mohamed Hussein "Mmachinga", Edibily Luny...

Mzee Akilimali asema, Clement Sanga anaihujumu Yanga

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Katibu wa Baraza la wazee la klabu ya Yanga, mzee Ibrahim Akilimali amesema kwamba, makamu kaimu mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga anaihujumu timu hiyo isifanye vizuri katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu. Akilimali ameyasema leo katika kipindi cha michezo cha Efm asubuhi, amedai Sanga amejiweka pembeni wakati timu ikiwa katika kipindi kigumu inachopitia. Amedai kiongozi huyo anataka kuona Yanga inashuka daraja ili lawama zote abebeshwe mzee Akilimali ambaye alimkataa Manji na sera yake ya kuikodisha Yanga. Katibu wa Baraza la wazee la Yanga,mxee Ibrahim  Akilimali

SIMBA MGUU SAWA KWA MBAO KESHO

Picha
Na Paskal Beatus. Mwanza Kikosi cha Simba kipo tayari kwa ajili ya mchezo wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji wao Mbao FC utakaopigwa kesho katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Simba iliwasiri Mwanza jana ikitokea Dar es Salaam ambapo iliifunga Mwadui FC ya Shinyanga mabao 3-0 huku Mbao FC ikitoka kupokea kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar mjini Morogoro hivyo mchezo wa kesho utakuwa mkali kwani Mbao hawatakubali kuendelea kupoteza mechi zake. Mbao FC wana kumbukumbu ya kufungwa na Simba mara mbili tatu ilizokutana, mara mbili kwenye Ligi Kuu na mara moja kwenye mchezo wa fainali ya kombe la FA, hivyo mchezo wa kesho utakuwa mgumu kwa timu mbili, Simba nao wanataka kushinda ili kukaa kileleni Simba wakiomba dua, kesho wanakutana na Mbao FC

Wachezaji Yanga warejea mazoezini

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Wachezaji wa mabingwa wa soka Tanzania bara, Yanga SC wamerejea mazoezini leo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza mgomo wao baridi uliochukua siku moja. Taarifa kutoka Jangwani zinasema wachezaji wamekubali kurudi mazoezini na uongozi unashughurikia malalamiko yao. Inasemekana wachezaji hao wanadai mishahara yao ya miezi miwili na ndio iliyopelekea mgomo huo. Yanga Jumamosi ijayo itachuana na Ndanda FC katika muendelezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara katika Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam Wachezaji wa Yanga wamerejea mazoezini leo baada ya mgomo wa siku moja

OKWI ALAMBA MILIONI MOJA YA UCHEZAJI BORA

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Mshambuliaji wa Simba SC, Emmanuel Okwi raia wa Uganda, amelamba kitita chake cha shilingi Milioni moja baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Mshambuliaji huyo alishinda tuzo hiyo baada ya kuisaidia timu yake kushinda mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting huku yeye akifunga mabao manne na kuseti moja. Okwi aliwabwaga nyota wenzake wawili, Mohamed Issa wa Mtibwa Sugar na Boniface Maganga wa Mbao FC. Emmanuel Okwi akippkea hundi ya shilingi milioni moja kutoka Vodacom

MANJI AWAAHIDI NEEMA WACHEZAJI YANGA,ASEMA ANARUDI

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Aliyekuwa mwenyekiti wa mabingwa wa soka nchini Yanga SC, Yusuf Mehbood Manji amewaahidi neema wachezaji wote wa Yanga na amedai haitachukua muda mrefu ataanza kuisaidia timu hiyo. Wachezaji wa Yanga na viongozi wao wote waliungana na Manji katika mahakama ya Kisutu juzi ambapo bosi huyo wa Quality Group alifikishwa hapo kujibu shitaka la kutumia dawa za kulevya, baada ya kuhairishwa kesi hiyo. Manji aliketi na nahodha wa Yanga, Nadir Haroub "Cannavaro" ambapo kati ya maneno waliyozungumza yamenaswa kuwa ni kumtaka mwenyekiti huyo wa zamani arejee kuokoa jahazi kitu ambacho alikubali. Manji alijiuzuru uenyekiti Yanga baada ya kuandamwa na matatizo na serikali kabla ya kufutiwa kesi yake ya kuhujumu uchumi hivyo sasa yuko huru na amewaambia wachezaji wa Yanga kwamba atarejea na raha zote zitarejea kama ilivypkuwa hapo nyuma. Wachezaji wa Yanga jana waligomea mazoezi katika uwanja wa Uhuru na inasemekana wanaidai klabu hiyo mishahara ya miezi m...

Wachezaji Yanga wagomea mazoezi kisa hawajalipwa chao

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Hali si shwari katika klabu ya Yanga baada ya wachezaji wake kugomea kufanya mazoezi leo ya asubuhi mpaka jioni yaliyokuwa yafanyike Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam na kujikuta wakielekea makao makuu mtaa wa Twiga na Jangwani. Yanga ilikuwa ifanye mazoezi yake leo ikiwa katika maandalizi yake ya Ligi Kuu Bara, inasemekana wachezaji wa Yanga walikataa kutelemka kwenye gari na kulazimika kufanya kikao na viongozi. Hata hivyo inasemekana wachezaji hao wameamua kugomea mazoezi kisa wanadai mishahara yao isiyopungua ya miezi miwili, uongozi wa Yanga haukuwa tayari kuzungumzia hilo ambapo kila mmoja alikuwa akimtupia mzigo mwenzake Wachezaji wa Yanga wamegoma kufanya mazoezi leo

Uongozi Simba wamkingia kifua Omog

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Uongozi wa klabu ya Simba umesema kocha wake mkuu,Mcameroon,Joseph Marius Omog ataendelea kukinoa kikosi hicho. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari Haji Sunday Manara ambapo amedai kocha huyo ataendelea na kazi yake na si kama wanavyotaka baadhi ya mashabiki wa timu hiyo ambao hawana uvumilivu. Manara amedai wapo baadhi ya mashabiki wanadhani kubadili makocha kila msimu ndio huleta mafanikio hilo si kweli na Omog atabaki kuwa kocha wa Wekundu hao ambao kwa sasa wanakamata nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Simba inajiandaa na mchezo wake ujao dhidi ya Mbao FC utakaofanyika jijini Mwanza kisha itaifuata Stand United mjini Shinyanga, awali mashabiki wa Simba walikuwa wakishinikiza kocha wao Joseph Omog aondolewe kwa sababu timu yao ilitoka suluhu na Azam FC Joseph Omog, aondoki kokote

Kocha wa Njombe Mji abwaga manyanga

Picha
Na Exipeditor Mataruma. Songea Kocha mkuu wa Njombe Mji FC ya Njombe, Hassan Banyai ameamua kubwaga manyanga baada ya mwenendo mbaya wa timu yake kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara. Banyai amejiuzuru baada ya timu yake kupoteza mechi zote tatu ilizocheza hadi sasa, kocha huyo aliyewahi kuzinoa Moro United na Majimaji ameamua kuacha kazi ili kumpisha kocha mwingine aweze kuwasaidia. Njombe Mji FC imefungwa mechi zote tatu za Ligi Kuu Bara, kitendo hicho kimepelekea kocha huyo kujiuzuru ili kulinda heshima yake kwani bado timu hiyo itaendelea kushindana na inaweza ku Hassan Banyai amebwaga manyanga

KISPOTI:

Picha
MIKONO YA NDUDA INALALAMIKA. Na Prince Hoza MASHABIKI na wapenzi wa Simba SC kuna wakati hawaeleweki kabisa, wao wanapenda starehe tu, shida ama taabu kwao si rafiki kabisa na hawataki kusikia kitu kama hicho, ukiwa na shida zako hawana habari na wewe wao wanachapa mwendo, hao ndio mashabiki wa Simba ambao wanacheka kwa dharau. Wanacheka kwa dharau kwa sababu timu yao kwa sasa ipo katika ubora wa hali ya juu, kikosi cha Simba kinaendeleza kutoa dozi kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Simba ilianza ligi kwa kishindo baada ya kuichapa Ruvu Shooting ya Mlandizi Pwani mabao 7-0 kabla haijalazimishwa sare isiyo ya mabao 0-0 na Azam FC ikiwa ni mechi yake ya kwanza kucheza ugenini, mechi hiyo ilipigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Dar es Salaam. Lakini mwishoni mwa wiki iliyopita, Simba iliivulumishia Mwadui FC ya Shinyanga mabao 3-0 mchezo uliopigwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, ushindi huo umeiwezesha Simba kufikisha pointi 7 na ikikamata ...

OKWI AKAMATIKI AISEE, AWAUA MWADUI YEYE NA BOCCO

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Simba SC imezidi kutoa vipigo vitakatifu baada ya jioni ya leo kuifanyia kitu mbaya Mwadui FC ya Shinyanga kwa kuichabanga bila huruma mabao 3-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Emmanuel Okwi "Muhenga" kama baadhi ya mashabiki wa mahasimu wao wanavyomuita, aliwainua vitini wapenzi na mashabiki wa Simba kwa kufunga mabao yake mawili safi huku nahodha, John Bocco "Adebayor" akitumbukiza moja na kuifanya Simba iibuke na ushindi huo mnono ikifikisha pointi saba na sasa inakamata nafasi ya pili. Katika mchezo huo wa leo vijana wa Simba wamecheza soka zuri na kufurahisha mashabiki wake ambapo Mwinyi Kazimoto na Jonas Mkude wakicheza kwa mara ya kwanza Emmanuel Okwi aliyevaa jezi namba saba akishangilia moja ya mabao yake