SIMBA YANG' ANG' ANIWA NA MBAO, CCM KIRUMBA
Na Paskal Beatus. Mwanza
Mabingwa wa Ngao ya Jamii, Simba SC jioni ya leo wameshikwa shati na Mbao FC baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba.
Simba ilitangulia kwa bao la winga Shiza Ramadhan Kichuya ambalo lilidumu hadi mapumziko, kipindi cha pili Mbao wakasawazisha kupitia mshambuliaji wake chipukizi Habibu Kiyombo kabla Simba hawasawazisha kupitia kiungo wake Mghana, James Kotei.
Mbao wakasawazisha kupitia kwa Emmanuel Mvuyekire kwa shati la mbali na kufanya matokeo yawe sare ambayo inawafanya Simba kubaki katika nafasi yao ya pili nyuma ya Mtibwa Sugar wenye pointi 9 huku Simba ikiwa na pointi 8.
Kwa matokeo hayo Simba itakuwa hatarini kupokwa nafasi hiyo na Azam FC au Singida United endapo zitashinda mechi zao za mwishoni mwa wiki, leo Emmanuel Okwi alipotezwa kabisa na vijana